• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Geita Town Council
Geita Town Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Geita

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Rasilimali Watu na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Afya, Ustawi wa jamii na Huduma ya Lishe
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Miundombinu, Maendeleo vijijini na Mjini
      • Usimamizi taka na Usafi wa Mazingira
    • Vitengo
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi Mazingira
      • Sheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Mawasiliano Serikalini
      • Usimamizi wa Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uchimbaji Madini
    • Sekta ya Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Afya, Ustawi wa jamii na Huduma ya Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Elimu na Afya
      • Kamati ya Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu ya Maombi
    • Miongozo
    • Jarida la Halmashauri
    • Mkakati wa kuziwezesha
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
  • Maeneo ya Uwekezaji

Shilingi Bilioni 2 Kujenga Uwanja wa Kisasa

Posted on: July 13th, 2021

Shilingi Bilioni 2 Kujenga Uwanja wa Kisasa

Halmashauri ya Mji wa Geita imeanza kutekeleza mradi wa ujenzi wa uwanja wa kisasa wa michezo katika mtaa wa Magogo Geita mjini ambapo katika awamu ya kwanza ya ujenzi jumla ya shilingi 2,040,312,754.92 za kitanzania  chanzo cha fedha ni  wajibu wa kampuni kwa jamii(CSR) kutoka mgodi wa GGM  zitatumika kutekeleza mradi huo.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kusaini mkataba wa ujenzi wa uwanja huo baina ya Halmashauri ya Mji wa Geita na mkandarasi EFQ Company Limited akishirikiana na Mugoo Construction Limited wa jijini Mwanza katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Geita hivi karibuni, Mkuu wa Wilaya ya Geita Mheshimiwa Wilson Shimo ameipongeza Halmashauri ya Mji Geita kwa maamuzi ya ujenzi wa uwanja wa kisasa wa michezo.

Mhe. Shimo amesema ana imani kuwa ushirikiano baina ya wakandarasi wawili utawezesha shughuli ya ujenzi wa uwanja kukamilika ndani ya kipindi kilichokubalika kwenye mkataba, kazi zinazowezekana kufanywa usiku na  mchana zifanyike bila visingizio vya aina yoyote ili uwanja huo uweze kuwanufaisha wakazi wa Geita na kuifanya tasnia ya michezo kuitangaza Halmashauri na fursa zilizomo ndani ya  Mji wa Geita.

Mkuu wa Wilaya ya Geita ametoa rai kwa wadau wa vyama vya michezo katika Wilaya ya Geita kuweka mkakati wa kuandaa timu nyingine za daraja la I ili ziendelee kuleta  hamasa ya michezo katika Wilaya ya Geita. Kadhalika wahakikishe timu ya Geita Gold ambayo  imepanda daraja na kuingia ligi kuu inanolewa, kutunzwa, kuboreshwa ili inapoingia ligi kuu isiwe na hofu ya kushuka daraja.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita Mhe. Costantine Morandi amewataka wakandarasi waliopata nafasi ya kujenga uwanja huo kufanya kazi haraka na  kwa weledi mkubwa  ili uwanja huo uweze kukamilika kwa wakati na kuwapatia fursa wananchi wa Geita kutazama mechi za timu yao wakiwa nyumbani. Pia ametoa sukrani za dhati kwa kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Geita (GGM) kwa ufadhili wao mkubwa katika sekta ya michezo na kuwasihi kuendeleza ushirikiano huo.

Halmashauri ya Mji wa Geita imetenga eneo lenye Hekta 10.4(104,570sqm) kwa ajili ya kujenga uwanja wa kisasa wa michezo ambao ndani yake kutakuwa na kiwanja cha mpira wa miguu, njia za mchezo wa riadha ,maeneo ya biashara na maegesho ya magari. Uwanja huo utakapokamilika utakuwa na uwezo wa wa kuingiza watazamaji 12,000 wote wakiwa wameketi.

Katika awamu ya kwanza ya ujenzi miundombinu muhimu itakayojengwa ni pamoja na Jukwaa kuu, kiwanja cha mpira wa miguu, vyumba vya wachezaji, chumba cha waamuzi, chumba cha kupima wachezaji,chumba cha huduma ya kwanza, Ofisi ya meneja wa uwanja na chumba cha mikutano, uzio wa ukuta wa tofali na milango ya kuingilia na uchimbaji wa kisima kirefu cha maji na matanki ya kuhifadhi maji kwa ajili ya ujenzi na matumizi ya uwanja.


Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI WA MAOHOJIANO (ORAL INTERVIEW) KADA YA MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II September 27, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA MAHOJIANO MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II September 29, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 05, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KATIKA USAHILI September 21, 2024
  • Zaidi

Habari Mpya

  • SERIKALI YAONGEZA FEDHA ZA ELIMU BURE MANISPAA YA GEITA

    May 11, 2025
  • WASIOFANYA USAFI KATIKA MAENEO YAO KUCHUKULIWA HATUA - DC KOMBA

    May 10, 2025
  • MAFUNZO KWA VIKUNDI VINAVYOTARAJIWA KUPEWA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI

    May 09, 2025
  • BURIANI MHE DAVID CLEOPA MSUYA

    May 07, 2025
  • Zaidi

Video

WATENDAJI WA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA WATAKIWA KUTOJIHUSISHA NA ITIKADI ZA KISIASA
More Videos

Kurasa za Karibu

  • Mfumo wa Watumishi kujihudumia
  • Applications Forms
  • Acts
  • Taarifa za Huduma za Afya
  • Mfumo wa Kupata Leseni za Biashara ( Mfumo wa Tausi)
  • Barua pepe za watumishi
  • Wasiliana nasi
  • Malalamiko
  • Taarifa za Mapato

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • TUWE MFANO KWA TAIFA' Yefred Myenzi
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Geita Tanzania

    Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita

    Namba ya Simu: 0282520437

    Mobile:

    Barua pepe: td@geitatc.go.tz

Mawasiliano Zaidi

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa