Mkurugenzi wa Manispaa ya Geita, Yefred Myenzi, amesema Serikali imeendelea kuwekeza fedha nyingi kuboresha sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu kama mabweni, madarasa, nyumba za walimu na vyoo, ili kuhakikisha mazingira rafiki ya kujifunzia na kufundishia.
Akizungumza katika mkutano wa tathmini ya maendeleo ya elimu kwa shule za sekondari, Myenzi amesema tangu kuingia madarakani kwa Rais Samia Suluhu Hassan, kumekuwa na mafanikio makubwa katika sekta ya elimu na afya.
"Tunampongeza Mheshimiwa Rais kwa namna alivyowekeza fedha nyingi za kuboresha miundombinu ya elimu.
Amesema licha ya ingezeko kubwa la wanafunzi bado kuna ongezeko la kiwango cha ufaulu uliofanya idara ya elimu kutoa tuzo kwa walimu waliofaulisha vizuri.
"Tunampongeza mweshimiwa Rais kwa namna alivyowekeza fedha nyingi za kuboresha miundo mbinu"
Amesema Geita inawanafunzi wengi hivyo bado Manispaa inafanya juhudi ya kuongeza miundombinu ya madarasa na nyumba za walimu.
"Serikali imewekeza sana katika elimu kwa kuhakikisha mazingira yanakuwa rafiki kwa wanafunzi na walimu, ili kufikia malengo ya taifa," amesema Myenzi.
Kwa mujibu wa Afisa Elimu Sekondari wa Manispaa hiyo, Rashid Muhaya, amesema Serikali imeongeza fedha za elimu bure kutoka Sh bilioni 1.07 mwaka 2021 hadi kufikia Sh bilioni 2.7 mwaka 2025.
Amesema kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Samia, idadi ya wanafunzi waliosajiliwa imeongezeka kutoka 17,145 mwaka 2021 hadi 22,362 mwaka huu, sambamba na kuongezeka kwa walimu, maabara, madarasa na shule mpya.
"Kwa miaka minne tumeona mabadiliko makubwa ambayo yamechochea ufaulu na kuimarisha utoaji wa elimu," amesema Muhaya.
Katika hafla hiyo, Divisheni ya Elimu ilitoa zawadi ya vyeti na fedha kwa shule zilizofanya vizuri kitaaluma, huku shule zilizofanya vibaya zikipatiwa mabango ya hamasa kwa lengo la kuzihimiza kuongeza juhudi.
Walimu walioshiriki mkutano huo pia walipata fursa ya kushiriki michezo mbalimbali kama njia ya kuimarisha mshikamano na kujenga upendo kazini.
TUFUATILIE KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII
Instagram
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa