SERIKALI imeidhinisha kiasi cha shilingi bilioni 7.7 kwa ajili ya kulipa madai na malimbikizo ya mishahara, likizo na masaa ya ziada kwa watumishi wa umma mkoani Geita kwa mwaka wa fedha 2025/26.
Mkuu wa mkoa wa Geita, Martine Shigella ametoa taarifa hiyo katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi 2025) kwa mkoa wa Geita yaliyofanyika mjini Geita.
Amesema mkoa wa Geita uliomba pesa hiyo na serikali iimeridhia kutoa pesa hiyo ili kuondoa malalamiko na kutengeneza mazingira rafiki ya wafanyakazi wakiwa ndani na nje ya ofisi za kazi.
Amesema ndani ya miaka minne sh bilioni 2.1 zimelipwa kama malimbikizo ya likizo na malipo ya muda wa ziada kazini huku sh bilioni 1.5 zimetumika kulipa malimbikizo ya mshahara kwa watumishi 4,323.
Ameongeza pia ndani ya miaka minne ya serikali ya awamu ya sita kwa kujali maslahi ya watumishi wa umma nchini takribani wafanyakazi 15,931 mkoani Geita wamepandishwa madaraja.
Amesema katika hatua nyingine watumishi 969 wa mkoa na halmashari zake wamebadilishiwa vitengo huku mkoa ukipokea watumishi wapya 8,426 kati yao 6,202 wakiwa ni walimu.
“Ndani ya kipindi cha miaka minne, wapo wafanyakazi 592 waliokwenda mafunzo ya muda mrefu, kati yao watumishi 501 wameenda mafunzo ya muda mrefu na wafanyakazi 91 wa muda mfupi”, ameeleza Shigella.
Amesema mabadiliko ya kada, vitengo na kielimu yemeendelea siyo tu kwa watumishi wa umma bali pia kwa sekta binafsi na kuitaja Kampuni ya Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML) kama mfano wa kuigwa.
Mtaalamu wa Usalama wa Mazingira GGML, Sia Malle amesema mgodi huo umelipa kipaumbele suala la usalama mahala pa kazi kwa kuzingatia matumizi ya vifaa vya kisasa kwa watumishi wote.
Mratibu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA), Magilu Ndembile aliiomba serikali kuendelea kufanyia kazi suala la kokotoo pamoja na uwasilishwaji wa michango katika mifuko ya kijamii.
TUFUATILIE KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII
Instagram
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa