Kituo cha Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC) kimetoa mafunzo ya uibuaji wa miradi inayoweza kutekelezwa kwa utaratibu wa ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) kwa Viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita
Mafunzo hayo ya uibuaji wa miradi inayoweza kutekelezwa kupitia ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) yametolewa leo Jumatano Aprili 02, 2025 na wakufunzi Dr Abiud Bongole na Christine kaigarula kutoka Kituo cha Ubia (PPPC)
Mafunzo hayo yamefanyika katika Ukumbi mdogo wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita
Katika mafunzo hayo, Dk Bongole ameeleza umuhimu wa PPP huku akishauri Halmashauri hiyo kutekeleza miradi mbalimbali kwa ubia.
Baada ya mafunzo hayo, wakufunzi hao kutoka PPPC kesho tarehe tarehe 03 Aprili, 2025 watatembelea na kuona baadhi ya miradi inayotekelezwa na inayotarajiwa kutekelezwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Geita
Kituo cha Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP Centre) kinaendelea kutoa mafunzo katika mikoa 13 nchini kwa ajili ya kusaidia uibuaji wa miradi inayoweza kutekelezwa kwa mfumo wa ubia.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa