Msimu Wa Pamba 2022/2023 Wazinduliwa Geita
Mkuu wa Wilaya ya Geita Mheshimiwa Wilson Shimo amezindua rasmi msimu wa kilimo cha Pamba 2022/2023 katika wilaya ya Geita ambapo amewashauri wakulima kuandaa mashamba yao mapema, kupanda mbegu bora, kutumia mbolea ya samadi Pamoja na na kuachana na safari zisizo za lazima msimu wa kilimo unapoanza.
Tukio la uzinduzi limefanyika tarehe 18/10/2022 katika Kata ya Bukondo wilayani Geita ambapo liliambatana na utoaji wa zawadi nav yeti vya pongezi kwa wakulima hodari ambao walifanya bidi katika shughuli za kilimo kwa msimu wa kilimo 2021/2022.
Akieleza mpango mkakati wa kuongeza tija katika zao la Pamba kwa msimu unaoanza, Mkaguzi wa Pamba wilaya ya Geita Bw. Ndinda Anthony ameeleza kuwa wilaya imejiwekea lengo la kulima ekari 30,000 za zao la Pamba zitakazozalisha kuanzia kilo 10,000,000 kwa kuzingatia masuala muhimu amnbayo ni kuimarisha upatikanaji wa zana za kilimo na pembejeo, kugawa malengo ya kilimo kulingana na uzalishaji wa maeneo kuanzia ngazi ya kiji/ Mtaa, kata, Tarafa hadi Halmashauri.
“ Tutaimarisha mfumo wa utoaji elimu na ushauri wa kilimo cha Pamba kwa kushirikiana na wakulima wawezeshaji wa vijiji au mitaa ili wakulima walime kwa kuzingatia kanuni bora za kilimo cha pamba, tutaanzisha mashamba darasa mawili kwa kila Kijiji yatakayomilikiwa na wakulima ili wakulima wengine waweze kujifunza kupitia mashamba hayo, kuwaunganisha wakulima wa zao la pamba Taasisi za Serikali na binafsi zinazotoa teknolojia za kilimo na ununuzi wa Pamba pamoja na kutoa motisha ya kutunuku zawadi wakulima hodari ili ushindani waw a kuzalisha kwa tija kubwa uendelee.” Aliongeza Ndg. Ndinda.
Wilaya ya Geita ina jumla ya kata 46 zinazolima zao la Pamba ambapo kwa msimu wa 2021/2022 kata ya Bukondo imeongoza kwa kutoa mkulima hodari na kuzalisha jumla ya kilo 349,000 za pamba ikifuatiwa na kata ya Butundwe ambayo imezalisha kilo 324,131 na ya tatu ni Kata ya Bulela iliyoko Halmashauri ya Mji Geita ambayo imezalisha kilo 213,627. Kwa ujumla uzalishaji wa zao la Pamba umeongezeka kuyoka kilo 1,639,638 msimu wa 2020/2021 hadi kili 3,339,333 kwa msimu wa 2021/2022.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa