Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Ndg. Gerson Msigwa amezitaka halmashauri zote nchini kuzingatia maelekezo ya Rais Samia kwamba vitengo vya mawasiliano ya serikali (GCU) viimarishwe kwa kupatiwa vitendea kazi na kwamba halmashauri ambazo hazitafanya hivyo zitakuwa zimekiuka maelekezo ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Ndg. Msigwa ametoa rai hiyo alipokuwa akifunga kikao kazi cha maafisa habari wa tawala za mikoa, halmashauri na taasisi zilizo chini ya TAMISEMI, kilichofanyika kwa siku mbili tarehe 23.05.2025 na 24.05.2025 kwenye Mji wa Serikali Mtumba - Dodoma ambapo pia amewasisitiza maafisa hao kutambua wajibu wao wa kufanya mawasiliano ya kimkakati hasa katika msimu huu wa uchaguzi mkuu ambapo upotoshaji kuhusu mambo mema na mazuri yaliyotekelezwa na serikali unaweza kuwa mwingi.
"Nakemea kasumba ya baadhi ya wakurugenzi wa halmashauri wanaodhani vitengo hivi havihitaji fedha. Katika masimu huu wa uchaguzi mkuu hakikisheni mnatumia redio za kijamii na waandishi wa habari kueleza mazuri ambayo serikali imeyatekeleza katika maeneo yenu.
" Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia Idara ya Habari mpaka sasa imeshafanya mikutano ya wanahabari (Press Conferences) na taasisi 35 za serikali hivi sasa ni zamu ya mawaziri kuvieleza vyombo vya habari mazuri ambayo wizara zao zimeyatekeleza kisha tarehe 16.06.2025 hadi 17.07.2025 itakuwa zamu ya wakuu wa mikoa yote nchini ambapo nao wataeleza mafaniko ya serikali katika mikoa. Hakikisheni mnashiriki kikamilifu katika kuandaa taarifa ambazo wakuu wenu wa mikoa wataziwasilisha mbele za wandishi wa habari". Alieleza kwa kina Msigwa.
Katika hatua nyingine, Ndg. Msigwa amewajulisha maafisa habari jukumu jipya la usimamizi na uratibu wa masuala ya mitandao ya kijamii ambalo Idara ya Habari Maelezo imekabidhiwa na kuwataka maafisa husika wenye mtanziko katika eneo hilo wawafikie ili kupata msaada na kuzilinda akaunti za taasisi zao dhidi ya watu wenye nia ovu wanaoweza kuzipora na kuzitumia vibaya kupotosha umma.
TUFUATILIE KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII
Instagram
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa