• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Geita Town Council
Geita Town Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Geita

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Rasilimali Watu na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Afya, Ustawi wa jamii na Huduma ya Lishe
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Miundombinu, Maendeleo vijijini na Mjini
      • Usimamizi taka na Usafi wa Mazingira
    • Vitengo
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi Mazingira
      • Sheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Mawasiliano Serikalini
      • Usimamizi wa Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uchimbaji Madini
    • Sekta ya Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Afya, Ustawi wa jamii na Huduma ya Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Elimu na Afya
      • Kamati ya Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu ya Maombi
    • Miongozo
    • Jarida la Halmashauri
    • Mkakati wa kuziwezesha
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
  • Maeneo ya Uwekezaji

MPANGO KABAMBE

Posted on: November 22nd, 2017

MPANGO KABAMBE WA MAENDELEO YA MJI GEITA KUINUA UCHUMI WA MKOA

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel amewataka wadau wa maendeleo ya Mkoa wa Geita kutumia fursa zinazopatikana katika mkoa huo na namna ya kuzitumia ili kuboresha maisha ya wananchi na kuinua uchumi kwa ujumla.

Akizungumza katika ufunguzi wa kikao cha kujadili mpango kabambe wa maendeleo ya Halmashauri ya Mji wa Geita 2017-2037 hivi karibuni katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji,  Mhandisi Robert Gabriel  amesema kuwa fursa kama uwepo wa eneo la kanda ya madini, maziwa makuu, misitu ya asili, bonde lenye rutuba kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji na barabara zinazounganisha mji huo na maeneo ya jirani zipangiwe mikakati itakayowakwamua wananchi kiuchumi.

“Mzingatie kuwa Halmashauri ya Mji Geita ndipo makao makuu ya Mkoa wa Geita na kitovu cha utawala na ukuaji wa uchumi wa mkoa ambapo shughuli zote za kiutawala, kijamii na kiuchumi zinafanyika, Hivyo Mpango kabambe ni muhimu kutekelezwa.” Aliongeza Mhandisi Robert Gabriel.

Mhandisi Robert Gabriel  amesema kuwa mji wa Geita unatoa soko la mazao kwa shughuli zinazofanyika katika wilaya hii, shughuli za usafirishaji, utalii, utawala, afya, elimu na benki hivyo ni vema uhusiano uliopo ukajadiliwa kwa kina ili kuleta chachu ya maendeleo kwa miji na maeneo yote yanayozunguka mkoa kwa ujumla.

Akieleza umuhimu wa mpango huo Mkuu wa Mkoa wa Geita amefafanua kuwa endapo mpango huo utatekelezwa vizuri utapunguza kero za viwanda vinavyotoa hewa chafu ambavyo viko pamoja na makazi ya watu, sehemu za kuabudia pamoja na maeneo ya starehe na baa zilizojengwa katikati ya makazi ya watu.

Afisa Mipango Miji wa Halmashauri ya Mji Geita Ndg. Oswald Cassian amesema kuwa mpango kabambe ni dira ya kuongoza, kusimamia na kudhibiti maendeleo ya ardhi kwenye sekta zote zinazotumia ardhi kama vile afya, elimu, barabara, maji, umeme, makazi/ viwanda  na mengineyo. Mpango huo ulianza kuandaliwa na Halmashauri kwa kushirikiana na wataalam kutoka Wizara ya Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi mwaka 2014.

Mji wa Geita ni moja kati ya miji 18 inayofadhiliwa na mradi wa ULGSP chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia, ambapo mpango kabambe ni moja ya mradi unaofanyika chini ya mpango huo. Kauli mbiu ya mpango huo ni “MPANGO KABAMBE WA MJI WA GEITA KATIKA KUSIMAMIA UENDELEZAJI WA RASLIMALI ZA MADINI YA DHAHABU”.



Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI WA MAOHOJIANO (ORAL INTERVIEW) KADA YA MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II September 27, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA MAHOJIANO MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II September 29, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 05, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KATIKA USAHILI September 21, 2024
  • Zaidi

Habari Mpya

  • BURIANI MHE DAVID CLEOPA MSUYA

    May 07, 2025
  • TWCC MKOA WA GEITA WAMEMKABIDHI HATI YA SHUKRANI MKURUGENZI MYENZI

    May 07, 2025
  • ZIARA YA MKUU WA WILAYA YA GEITA MHE. HASHIM A KOMBA KUTEMBELEA NJIA NA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE WA UHURU 2025

    May 06, 2025
  • KAMATI YA FEDHA NA UONGOZI YAMPONGEZA MKURUGENZI MYENZI

    May 05, 2025
  • Zaidi

Video

WATENDAJI WA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA WATAKIWA KUTOJIHUSISHA NA ITIKADI ZA KISIASA
More Videos

Kurasa za Karibu

  • Mfumo wa Watumishi kujihudumia
  • Applications Forms
  • Acts
  • Taarifa za Huduma za Afya
  • Mfumo wa Kupata Leseni za Biashara ( Mfumo wa Tausi)
  • Barua pepe za watumishi
  • Wasiliana nasi
  • Malalamiko
  • Taarifa za Mapato

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • TUWE MFANO KWA TAIFA' Yefred Myenzi
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Geita Tanzania

    Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita

    Namba ya Simu: 0282520437

    Mobile:

    Barua pepe: td@geitatc.go.tz

Mawasiliano Zaidi

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa