MNEC Apongeza Hatua Za Ujenzi Wa Uwanja Wa Michezo
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Geita Ndugu Evarist Gervas ametoa pongezi za dhati kwa uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Geita na Mgodi wa Dhahabu Geita kwa utekelezaji unaoridhisha wa ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa kisasa unaojengwa katika mtaa wa Magogo Geita mjini.
Ndg. Evarist ametoa pongezi hizo hivi karibuni wakati wa ziara yake ya kutembelea utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa madarasa, shule mpya, vituo vya afya, zahanati ambayo imejengwa ndani ya kipindi cha siku 365 za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Mji wa Geita
“Nimeridhishwa na hatua ya maendeleo ya ujenzi wa uwanja huu. Mkurugenzi pamoja na timu yako pamoja na Mgodi wa GGM ambao ndio wawezeshaji katika utekelezaji wa ujenzi wa mradi huo. Niwasihi muendeleze juhudi hizi ili kuhakikisha ujenzi unaisha kwa wakati uliopangwa na kuhakikisha timu yetu ya Geita Gold inaanza kucheza kwenye uwanja wa nyumbani na kuwapa fursa wakazi wa Geita kutazama mechi kubwa Mkoani kwao.” Aliongeza Evarist Gervas.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita Bi. Zahara Michuzi amesema kuwa ujenzi wa uwanja wa kisasa wa michezo umefikia asilimia 65 na Halmashauri yake imejipanga kukamilisha ujenzi huo kwa awamu ya kwanza mwezi mei 2022 ili uweze kutumika kwa michezo ya mpira na wanageita waweze kuutumia kwa kufanya mazoezi ya viungo.
Ujenzi wa uwanja wa michezo Magogo unajengwa na mkandarasi EFQ COMPANY LTD na MUGOO CONSTRUCTION COMPANY LIMTED kwa gharama ya Shilingi 2,407,569,050.81 kwa awamu ya kwanza ambapo mundombinu inayojengwa ni pamoja na Ujenzi wa ukuta, mtaro wa maji ya mvua, jukwaa kuu,njia za mchezo wa riadha na uwanja wa kchezea mpira(pitch)
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa