Mkurugenzi wa Manispaa ya Geita, Ndugu Yefred Myenzi, akiambatana na timu ya Mapato Manispaa ya Geita, amefanya ziara ya kutoa elimu kwa wachimbaji wadogo kuhusu ulipaji wa kodi na tozo mbalimbali za serikali. Ziara hiyo imelenga kuongeza uelewa kwa wadau wa sekta ya madini juu ya wajibu wao katika kuchangia pato la Halmashauri na taifa pia.
Maeneo yaliyotembelewa ni pamoja na:
- Moroko (Mtaa wa Nyantorontoro A)
- Nyamatagata (Kata ya Mgusu)
- Mgusu Miners (Kata ya Mgusu)
Akiwa katika ziara hiyo, Mkurugenzi Myenzi amewapongeza wawekezaji kwa namna wanavyowekeza kwenye sekta ya uchimbaji kwa kutumia vifaa vya kisasa pamoja na kutoa ajira kwa vijana, hivyo kuchangia pato la jamii na ustawi wa wananchi.
Aidha, amewapongeza kwa maandalizi mazuri ya taarifa za mauzo pamoja na uwazi katika ulipaji wa tozo mbalimbali za serikali.
Mkurugenzi Myenzi amesisitiza kuwa uwazi katika ulipaji wa kodi ni jambo la msingi, kwani kukwepa kodi ni kurudisha nyuma juhudi za maendeleo na kuikosesha serikali mapato ya kutekeleza miradi ya huduma za kijamii.
Amewasihi wachimbaji wote kutambua wajibu wao katika kuijenga Geita na taifa kwa ujumla kupitia ulipaji wa kodi kwa hiari.
TUFUATILIE KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII
Instagram
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa