Mkurugenzi wa Mji Ndg. Yefred Myezi, amewahasa wananchi kutouza chakula chote ili kujikinga na baa la njaa.
Mkurugenzi Myenzi ameyasema hayo wakati wa ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe. Komba alipotembelea Kata ya Ihanamilo ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kutembelea Kata zote za Halmashauri ya Mji Geita iliyoanza jana katika Kata ya Nyanguku kwa ajili ya kujitambulisha, kuijua Halmashauri ya Mji wa Geita, Kutembelea na kukagua miradi iliyokwama ili iweze kukamilishwa na kuanza kutoa huduma lakini pia kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia majibu.
Mkurugenzi Myenzi amesema tumepita maeneo mengi na kutokana na mvua nyingi chakula kingi kimepatika lakini tusikiuze chote kuepukana na baa la njaa
Wakati huo huo, Mhe Komba amekagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Nyakahengele, mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Igenge, mradi wa ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) katika Zahanati ya Bunegezi na kufanya mkutano wa hadhara katika Mtaa wa Ikulwa.
Wakati wa mkutano wa hadhara ilimradhimu Mhe. Komba kusitisha mkutano kwa muda na kwenda katika Kijiji cha Wigembya kujionea hali halisi ya mradi wa maji uliokuwa ujaanza kutoa huduma kwa wananchi na kuziagiza Taasisi za RUWASA na GEUWASA kuhakikisha mradi huo unaanza kutoa huduma mara moja BONYEZA HAPA KUONA VIDEO
Katika ziara hiyo, Mhe. Komba aliambatana na Katibu Tawala Wilaya, Kamati ya Usalama Wilaya, Mkurugenzi wa Mji, Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Mji, Afisa Tarafa ya Geita na Wakuu wa Taasisi za TANESCO, TARURA na GEUWASA na ziara hii itaendelea kesho katika Kata ya Mgusu
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa