Suala la mkopo wa asilimia 10 unaotolewa na Halmashauri linazidi kuwa ni matumaini makubwa baada ya kundi kubwa la walionufaika kupiga hatua katika shughuli zao na wao kuajiri wengine.
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Ndg. Mohammed Ali Kawaida (MCC) akiwa na Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Ndg. Rehema Sombi Omary na Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji tarehe 28, 28 2025 wakiwa katika ziara ya kikazi wilaya ya Geita wametembelea kikundi cha Vijana cha Maisha ambacho kinajishughulisha na kuzalisha mikanda ya Gypsum kilichopo kata ya Nyankumbu.
Akiwa katika Kiwanda hicho Ndg. Kawaida alipokea taarifa yao ambapo wameeleza walianza na mtaji wa Shilingi milioni 7.8 wakiwa na uwezo wa kuzalisha mikanda 1,500 kwa wiki na baada ya kuchukua mkopo halmashauri mwaka 2021/2022 wa Shilingi milioni 40 waliweza kuzalisha mikanda 4,800 kwa wiki.
Pia wameeleza mahitaji yalizidi ndipo Oktoba 2024 waliweza kuzalisha mikanda milioni 2,160,000 iliyoweza kusaidia kuripa marejesho na Novemba 2024 wakapata mkopo mwingine wa Shilingi milioni 110 ambao umewafanya kuongeza uzalishaji wa mikanda na kufikia milioni 4,000,000 kwa mwaka.
Kikundi hicho kimepata soko kubwa za bidhaa zao katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Kigoma na Kagera pia mashirika, Serikali na watu binafsi huku kikitoa ajira kwa vijana 20 ambao maisha yao yamebadilika kutokana na kipato wanachopata.
Ndg. Sombi alipopata nafasi ya kuzungumza aliwapongeza kwa kuzalisha ajira na kuwa na nidhamu ya fedha ambayo imewafanya biashara yao kukua na ametoa rai kwa Maofisa Maendeleo ya Jamii kutokaa ofisini na badala yake watoe elimu ili vijana wengi wapate mkopo huo.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa