WAKULIMA WATAKIWA KUTUMIA KANUNI BORA ZA KILIMO CHA PAMBA
Wakulima wa pamba Mkoani Geita wametakiwa kufuata kanuni bora za kilimo cha zao hilo ili kupata mazao yenye tija na kufanya kilimo hicho kuwa cha biashara.
Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Luhumbi alipokuwa akizindua msimu wa kilimo cha pamba kwa Mkoa wa Geita katika mashamba ya watumishi wa Halmashauri ya Mji yaliyoko kata ya Buhalahala.
Mhandisi R. Luhumbi amesema kuwa kanuni ambazo wakulima wanatakiwa wazifuate ni kutayarisha mashamba mapema, kutumia mbolea za samadi na virutubisho vingine, kupanda pamba mapema kwa mistari na nafasi maalum, kunyunyiza madawa ya kuzuia wadudu waharibifu, kuvuna na kuchambua pamba mapema, kung’oa na kuchoma moto masalia yote ya pamba.
Mkuu wa Mkoa wa Geita pia amewaagiza Maafisa kilimo kuwafuatilia kwa karibu wakulima wa pamba na kuwaelekeza kulima kwa tija ili kuzalisha Zaidi tofauti na miaka ya nyuma.
Lengo ni kuongeza tija ya uzalishaji kutoka wastani wa kilo 250 hadi 300 mpaka wastani wa kilo 800.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa