Hayo yamebainishwa leo tarehe 24 Julai, 2024 wakati wa Mkutano wa Tume Huru ya Uchaguzi na Wadau wa Uchaguzi wa Mkoa wa Geita kuhusu Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, uliofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita.
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imetoa wito kwa wananchi na wapiga kura wa mkoa wa Geita kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kuboresha taarifa zao kwenye uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unaotarajiwa kufanyika kwenye mkoa huu kuanzia tarehe 05 hadi 11 Agosti, 2024.
Akifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoani Geita, leo Agosti 24, 2024, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele amesema uboreshaji huu unamhusu kila mwananchi mwenye sifa ya kuandikishwa kuwa Mpiga Kura.
“Ni vyema mkatambua kuwa uboreshaji huu unamhusu kila mwananchi mwenye sifa ya kuandikishwa kuwa mpiga kura na anayeboresha taarifa zake. Hivyo, natoa rai kwenu kuwahimiza wananchi kupitia majukwaa yenu ya kisiasa, kijamii, kitamaduni, kiimani na kiuchumi wajitokeze kwa wingi kujiandikisha na kuboresha taarifa zao kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura,” alisema Jaji Mwambegele.
Akiwasilisha mada wakati wa mkutano huo, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima, R. K, amesema kwa mkoa wa Geita Tume inatarajia kuandikisha wapiga kura wapya 299,672.
“Hii ikiwa ni ongezeko la asilimia 24.7 ya wapiga kura 1,212,146 waliopo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Hivyo, Tume inatarajia baada ya uandikishaji Mkoa wa Geita utakuwa na wapiga kura 1,511,818,” alisema Bw. Kailima.
Aidha, Kailima ameongeza kuwa kwa lengo la kutekeleza jukumu hilo kwa ufanisi, uboreshaji kwa awamu ya kwanza utafanyika kwenye mizunguko 13 kama ilivyobainishwa kwenye ratiba Tume.
“Zoezi hili litaendeshwa kwa siku saba kwenye kila kituo cha kuandikisha wapiga kura. Tunatarajia zoezi litakamilika Machi, 2025,” amesema Bw. Kailima.
Mkutano huu una lengo la kuwapa wadau taarifa za uwepo wa zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na kuwapitisha katika vifaa na mifumo ya uandikishaji pamoja na kuona namna zoezi litakavyofanyika vituoni.
Uboreshaji huu wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unaenda sambamba na kauli mbiu inayosema;
"Kujiandisha kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora"
PICHA MBALIMBALI KATIKA MATUKIO
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa