Waziri wa Nchi, Ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Selemani Jafo amesema Halmashauri ya Mji wa Geita imeongoza kwa ukusanyaji mapato kwa mwaka wa fedha 2017/18 kati ya halmashauri zote nchini.
Waziri Jafo amesema hayo wakati akitoa taarifa ya makusanyo ya mapato ya Halmashauri zote nchini Mkoani Dodoma
Waziri Jafo atangaza Makusanyo ya Halmashauri za Mikoa, Wilaya, miji na majiji.
Waziri amesema kuwa serikali imekuwa ikifuatilia ukusanyaji wa Mapato katika Halmashauri zote ili kuweza kufanikisha utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo katika Halmashauri zote nchini.
Halmashauri ya Mji Geita imekusanya Tsh 6,863,169,216 Sawa na 218% katika Mwaka wa Fedha 2017/2018.
Waziri Jafo amesema kila Halmashauri nchini itapimwa kwa Kiwango cha ukisanyaji Mapato
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa