Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassimu Majaliwa amefurahishwa na kuridhishwa
na miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika Halmashauri ya Mji wa Geita
ambapo hadi kukamilika kwake itagharimu zaidi ya 8.5 Bilioni.
Mhe. Kassimu Majaliwa amedhihirisha hayo alipotembelea miradi ya ujenzi wa soko kuu la Geita Mjini na ofisi za halmashauri za mji huo,
Alisema Soko jipya ambalo linatarajiwa kufunguliwa rasmi mwezi januari mwakani ambalo
litatumiwa na wafanyabiashara 200 ni fursa nzuri ya kuinua uchumi wa mji huo.
Alisema pia
ameridhishwa na mkakati uliowekwa kuhakikisha, wale wote ambao walikuwa na vibanda katika
soko la zamani,wanapewa maeneo mapya.
Akizungumzia ujenzi wa majengo mapya ya halmashauri ya mji wa Geita,
alieleza kuridhishwa na mradi huo ambao sasa yamegharimu kiasi cha 2.5 bilioni katika awamu ya kwanza
na hadi jengo kukamilika utagharimu 6.6 bilioni.
Awali Mkuu wa mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel alisema halmashauri ya mji wa Geita ,
imejipanga kufanya mabadiliko makubwa ya mji ambao sasa utakuwa moja ya miji bora nchini lakini pia
kuendelea kuongoza kwa kukusanya mapato.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Geita, Leonard Lugomola alisema wamejipanga kuhakikisha
wakazi wa Geita wananufaika kutokana na fedha za ndani na serikali.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa