Hayo yamedhihirishwa tarehe 08 Februari, 2025 katika bonaza la Watumishiwa Idara ya Afya lililowahusisha watumishi wa Idara za Afya kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Geita na Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana (Sekou Toure) lililofanyika katika viwanja vya Shule ya Wasichana ya Sekondari ya Nyankumbu.
Katika bonaza hili lililoshirikisha michezo mbalimbali na matokeo yake yakiwa kama ifuatavyo; kwa upande riadha mita 100 timu ya wanawake kutoka Geita iliongoza na upande wa wanaume kutoka Geita waliongoza pia
Kwa mchezo wa kukimbia na magunia timu za wanawake na wanaume kutoka Geita ziliongoza katika mchezo huu, kwa mchezo wa Kukimbia na Mayai kwenye Kijiko timu za wanawake na wanaume kutoka Geita ziliongoza.
Kwa mchezo wa kuvuta Kamba timu za wanawake na wanaume kutoka Geita ziliibuka kidedea, katika Kukimbiza Kuku timu ya wanawake Geita iliibuka mshindi huku upande wa wanaume Sekou Toure wakiondoka na ushindi.
Kwa upande wa draft wanaume wa Geita waliongoza ushindi huku upande wa Karata timu ya wanawake kutoka Geita iliongoza na kwa upande wa wanaume Sekou Toure walijinyakulia ushindi.
Vile vile kwenye mchezo wa mpira wa nyavu (netball) Geita imeshinda goli 20 kwa 15 dhidi ya Sekou Toure wakati mpira wa miguu zikitoka kwa sare ya goli moja kwa moja
Ushiriki wa Bonaza hili ni muendelezo wa urafiki kati ya Manispaa ya Geita na Wilaya ya Nyamaga ambapo itakumbukwa tarehe 01 Februari, 2025 Manispaa ya Geita ilialikwa katika bonaza lililofanyika katika viwanja vya Butimba TTC Wilayani Nyamagana ambapo Geita iliiburuza Wilaya ya Nyamagana kwa kushinda michezo yote mitatu.
MATUKIO KATIKA PICHA
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa