Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita Ndg. Yefred Myenzi wa kwanza kushoto akiwa na wakurugenzi wenzie kwenye uzinduzi wa sera ya Elimu
Uzinduzi huo wawa sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 toleo la 2023 umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete uliopo Dodoma leo tarehe 1 Februari, 2025
Uzinduzi huo uliambatana na kauli mbiu inayosema "elimu na ujuzi ndio mpango mzima"
Pamoja na mambo yote, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ndiye mgeni rasmi katika uzinduzi huu amesema kupitia sera mpya ya elimu inankwenda kuwasaidia vijana kupata fursa mbalimbali katika soko la ajira kutokana uwepo wa mikondo ya ufundishaji somo la lugha ya Kichina, Kifaransa na Kiarabu.
Rais Dkt. Samia amesema kuwa lugha ya kingereza itaendelea kufundishwa lakini pia yameongezwa masomo hayo ya lugha ya Kichina, Kifaransa na Kiarabu.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa