Mashindano ya michezo kwa shule za sekondari katika Halmashauri ya Manispaa ya Geita yamefanyika kwa mafanikio makubwa, yakiwa na lengo la kuimarisha elimu, afya na mshikamano wa wanafunzi kupitia kauli mbiu: “Tukutane Shuleni, Tujenge Kesho Iliyo Bora.”
Kauli mbiu hii imebeba dhamira ya kumuunga mkono Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika juhudi zake za kuendeleza elimu na maendeleo ya vijana nchini.
Jumla ya shule 40 (shule 30 za Serikali na 10 binafsi) zimeshiriki kwenye mashindano haya, ambayo yamejikita katika malengo yafuatayo:
- Kuhamasisha wanafunzi kuendelea na masomo
- Kupunguza utoro na kuongeza mahudhurio shuleni
- Kuibua na kuendeleza vipaji vya wanafunzi
- Kukuza mshikamano wa kijamii
- Kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa lishe bora na elimu
Mkurugenzi wa Manispaa ya Geita, Ndugu Yefred Myenzi, katika hotuba yake aliipongeza idara ya elimu na walimu kwa maandalizi mazuri. Alisema:
“Hii ni ishara tosha kuwa Geita tunathamini maendeleo ya elimu kwa njia zote ikiwemo michezo. Ushirikiano baina ya walimu, wanafunzi, jamii na viongozi umetufikisha hapa, kama Manispaa, tutaendelea kuweka mazingira bora ya kuendeleza vipaji hivi kwa manufaa ya vijana na taifa kwa ujumla.”
Aidha, aliendelea kuomba kampuni ya GGML kuendelea kudhamini shughuli hizi za michezo kila inapohitajika ili kusaidia kuinua vipaji vya watoto wetu.
Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mhe. Hashim A. Komba, ambaye alikuwa mgeni rasmi, alieleza kuwa:
“Mashindano haya yameonesha wazi kuwa michezo si burudani tu, bali ni sehemu ya kujenga nidhamu, kuimarisha afya, kuibua vipaji na kuhamasisha ushiriki wa wanafunzi mashuleni, kama Wilaya tunajivunia kuona jinsi shule zetu zilivyoshiriki kwa ari kubwa.”
Alihitimisha kwa kusisitiza umuhimu wa kuendeleza vipaji vilivyojitokeza kwa kuwapatia malezi na mafunzo stahiki, ili waweze kuwa wachezaji bora wa baadaye katika ngazi ya taifa na kimataifa.
TUFUATILIE KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII
Instagram
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa