• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Geita Town Council
Geita Town Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Geita

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Rasilimali Watu na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Afya, Ustawi wa jamii na Huduma ya Lishe
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Miundombinu, Maendeleo vijijini na Mjini
      • Usimamizi taka na Usafi wa Mazingira
    • Vitengo
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi Mazingira
      • Sheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Mawasiliano Serikalini
      • Usimamizi wa Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uchimbaji Madini
    • Sekta ya Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Afya, Ustawi wa jamii na Huduma ya Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Elimu na Afya
      • Kamati ya Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu ya Maombi
    • Miongozo
    • Jarida la Halmashauri
    • Mkakati wa kuziwezesha
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
  • Maeneo ya Uwekezaji

MAPATO YAONGEZEKA MANISPAA YA GEITA SHILINGI BILIONI 5 KWA MWAKA MMOJA

Posted on: May 13th, 2025

Baraza la Madiwani la Manispaa ya Geita limempongeza Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Yefred Myenzi, kwa mafanikio makubwa ya kuongeza makusanyo ya mapato ya ndani kutoka Sh bilioni 14 hadi Sh bilioni 19 ndani ya mwaka mmoja wa uongozi wake.

Pongezi hizo zimetolewa leo Mei 13, 2025, katika kikao cha robo ya nne ya baraza hilo lililoanza kazi mwaka 2020 na kuhitimisha kazi yake Mei 2025 .

Mbali na pongezi hizo kikao hicho pia kilijadili mafanikio mengine yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wao.

Akizungumza kwenye kikao hicho, Meya wa Manispaa ya Geita, Constantine Morandi, alisema mafanikio hayo yametokana na usimamizi madhubuti wa mifumo ya ukusanyaji mapato uliosimamia na Mkurugenzi.

 “Ongezeko la Sh bilioni tano kwa mwaka mmoja ni jambo kubwa. Vyanzo vya mapato ni vilevile, lakini mapato yameongezeka. Hii inaonyesha wazi kuwa Mkurugenzi amesimamia vizuri ukusanyaji mapato hatujaongeza vyanzo vya mapato ni vilevile lakini kunaongezeko la Sh Bilion tano,” amesema Morand.

Ameongeza kuwa Mkurugenzi Myenzi amekuwa mfano wa kuigwa kwa uwajibikaji na utendaji bora uliosaidia kuleta maendeleo katika Manispaa hiyo.

Katika kipindi cha miaka mitano, mapato ya ndani ya halmashauri hiyo yameongezeka kutoka Sh bilioni 8 mwaka 2020 hadi kufikia Sh bilioni 19 mwaka huu.

Mafanikio mengine yaliyoelezwa na Meya huyo ni pamoja na ujenzi wa shule mpya, vyumba vya madarasa zaidi ya 400, matundu ya vyoo zaidi ya 420, na maabara mpya 16 kwa shule za msingi na sekondari.

Katika sekta ya afya, vituo vya afya vimeongezeka kutoka kimoja mwaka 2020 hadi kufikia vitano – vinne vikiwa tayari vimekamilika na kimoja kikiwa hatua za mwisho za ujenzi.

Aidha, mikopo kwa wanawake, vijana na makundi maalum kupitia asilimia 10 ya mapato ya ndani imeongezeka kutoka Sh milioni 698 mwaka 2020 hadi kufikia Sh bilioni 1.78 mwaka huu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Yefred Myenzi amesema zaidi ya Sh bilioni 3 zilitolewa na Serikali Kuu kwa kipindi  cha robo ya nne ya mwaka kwa ajili ya miradi mbalimbali ya madeleo.

Amesema matumizi ya fedha hizo ni pamoja na utekelezaji wa miradi ya  TASAF, Mfuko wa Jimbo na ujenzi wa kituo cha ualimu kinachojengwa katika kata ya Kalangalala

Ameeleza pia kuwa Manispaa hiyo inaendelea kutekeleza miradi ya CSR yenye thamani ya Sh milioni 422, ambapo Sh milioni 204 tayari zimepokelewa na miradi 18 kati ya 34 imekamilika.

Kuhusu mitihani ya kidato cha sita, Myenzi amesema jumla ya watahiniwa 934 wamesajiliwa, wakiwemo 61 wa kujitegemea, na hadi sasa hakuna changamoto yoyote iliyojitokeza.

Kuhusu hali ya chakula aamesema tathmini ya chakula kwa sasa inaonesha hali ni shwari, hakuna dalili za njaa, huku ujenzi wa kituo kikuu cha mabasi ukitarajiwa kuanza mwezi Juni baada ya mkandarasi kusaini mkataba.

Akigusia afya ya jamii, Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa wagonjwa 30 walibainika kuwa na vimelea vya ugonjwa wa Ipox, ambapo 29 wamepona na watatu wanaendelea na matibabu.

Myenzi amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari.

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA









TUFUATILIE KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII
Instagram

Facebook

X

Youtube

Matangazo

  • TANGAZO KUHUSU FURSA ZA MIKOPO YA ASILIMIA 10 May 27, 2025
  • Zaidi

Habari Mpya

  • MJI WETU UWE SAFI HII ITATUEPUSHA NA MAGONJWA - DC KOMBA

    May 31, 2025
  • GEITA MANISPAA YAADHIMISHA SIKU YA WAUUGUZI NA WAKUNGA

    May 30, 2025
  • GEITA MANISPAA YAADHIMISHA SIKU YA WAUUGUZI NA WAKUNGA

    May 30, 2025
  • WANANCHI WANAHITAJI TAARIFA SAHIHI, KWA WAKATI NA ZENYE KUELEWEKA KUHUSU MIRADI YA MAENDELEO

    May 25, 2025
  • Zaidi

Video

WATENDAJI WA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA WATAKIWA KUTOJIHUSISHA NA ITIKADI ZA KISIASA
More Videos

Kurasa za Karibu

  • Mfumo wa Watumishi kujihudumia
  • Applications Forms
  • Acts
  • Taarifa za Huduma za Afya
  • Mfumo wa Kupata Leseni za Biashara ( Mfumo wa Tausi)
  • Barua pepe za watumishi
  • Wasiliana nasi
  • Malalamiko
  • Taarifa za Mapato

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Geita Tanzania

    Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita

    Namba ya Simu: 0282520437

    Mobile:

    Barua pepe: td@geitatc.go.tz

Mawasiliano Zaidi

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa