Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Geita kupitia Idara ya Utumishi na Utawala, iliandaa hafla maalum ya kuwaaga rasmi watumishi waliostaafu utumishi wa umma. Sherehe hiyo ilifanyika Ijumaa, tarehe 01 Agosti 2025, katika ukumbi wa GEDECO.
Hafla hiyo iliongozwa na Mkurugenzi wa Manispaa, Ndugu Yefred Myenzi, akishirikiana na watumishi kutoka Idara ya Utawala, ambapo walitoa heshima kwa wastaafu kwa kazi yao ya muda mrefu iliyojengwa juu ya misingi ya uadilifu, uwajibikaji na uzalendo.
Katika hotuba yake, Mkurugenzi Myenzi aliwapongeza wastaafu kwa utumishi wao uliotukuka na mchango mkubwa walioutoa kwa maendeleo ya Manispaa. Aliwatakia maisha yenye afya, amani na baraka katika safari yao mpya ya maisha ya kustaafu. Pia aliwahimiza watumishi waliobaki kuendelea kujifunza kwa kuiga mfano mzuri waliouacha wastaafu, huku wakidumisha bidii na uaminifu kazini.
Kwa kutambua na kuthamini mchango wao, wastaafu walikabidhiwa zawadi maalum kama ishara ya upendo, heshima na shukrani kutoka kwa uongozi pamoja na wafanyakazi wenzao. Sherehe hiyo iliambatana na burudani mbalimbali na chakula cha pamoja kilichoashiria mshikamano na mahusiano mema.
Manispaa ya Geita inaahidi kuendelea kudumisha ushirikiano na mahusiano bora na watumishi wake waliostaafu, ikitambua kuwa mchango wao bado ni muhimu kwa jamii.
TUFUATILIE KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII
Instagram
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa