Halmashauri ya Manispaa ya Geita kupitia Mkutano wake wa Baraza la Madiwani wa robo ya pili Oktoba hadi Desemba kwa mwaka wa fedha 2024/2025 uliofanyika katika Ukumbi wa EPZ leo tarehe 7 February, 2025 imemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha nyingi kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo.
Pamoja na shukrani zilizotolewa Baraza limemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu kwa kuipandisha hadhi Halmashauri kutoka Halmashauri ya Mji hadi kuwa Halmashauri ya Manispaa.
Mkutano wa huu Kawaida wa Baraza la Madiwani, Waheshimiwa Madiwani waliwasilisha Taarifa za Utekelezaji wa shughuli zilizofanyika kwenye Kata zao kwa kipindi cha Robo ya pili Oktoba hadi Desemba 2025 pamoja na kupitia na kujadili taarifa za Kamati mbalimbali za kudumu za Halmashauri.
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHAMkurugenzi wa Halmshauri ya Manispaa ya Geita Ndg. Yefred Myenzi akifafanua jambo
Naibu Meya wa Halmshauri ya Manispaa ya Geita Mhe. Elias C Ngole akifafanua jambo
DIwani Viti Maalum Mhe. Diana akiwasilia Taarifa ya utekelezaji
Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi katika Halmshauri ya Manispaa ya Geita Ndg. Sostenes Mbwilo akifafanua jambo
Waheshimiwa Madiwani, Wajumbe na Wageni waalikwa katika Baraza hilo wakifuatilia mkutano wa huo
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa