Watumishi wa Idara ya Afya Halmashauri ya Manispaa ya Geita leo tarehe 01 Februari, 2025 wamewaburuza watumishi wa Idara ya Afya Wa Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana katika michezo mitatu tofauti iliyochezwa katika viwanja vya Butimba TTC Wilayani Nyamagana
Ushiriki wa michezo hii umetokana na mwaliko kutoka kwa watumishi wa Idara ya Afya Hospitali ya Nyamagana ambapo Halmashauri ya Manispaa ya Geita ilialikwa kupitia Hospitali yake ya Manispaa inayosimamiwa na Idara ya Afya na Huduma za Lishe
Michezo iliyochezwa ni pamoja na mpira wa miguu kwa wanaume, mpira wa nyavu (netball) kwa wanawake na volleyball kwa wanawake. Ambapo katika kila mchezo Halmashauri ya Manispaa ya Geita iliibuka mshindi kwa upande wa mchezo wa mpira wa miguu kwa wanaume Geita imeshinda goli 3 kwa 2 dhidi ya nyamagana, mpira wa nyavu (netball) kwa wanawake Geita imeshinda goli 20 kwa 0 dhidi ya Nyamagana na volleyball kwa wanawake imeshinda seti 2 kwa 1 dhidi ya Nyamagana.
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa