Akizunguma Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Ndugu. Robert Sungura amesema jumla ya vikundi 100 vyenye wanachama 503 wanawake wakiwa 387,Wanaume 116 kwenye makundi ya Wanawake,Vijana na Watu wenye ulemavu,
Vikundi vya Wanawake 57 wanapatiwa mikopo yenye thamani ya shilingi milioni 550,Vikundi vya Vijana 38 wanapatiwa mikopo yenye thamani ya zaidi ya milioni 622 na Vikundi 5 vya watu wenye ulemavu vinapatiwa mikopo yenye thamani ya shilingi milioni 56.
Amesema wameweka mikakati ya kuimarisha mfumo wa usimamizi na ufuatiliaji wa marejesho ili kuendelea kubaini baadhi ya vikundi vyenye viashiria vya kusambaratika hii itasaidia kuchukua hatua kwa wakati pia wanaendelea kutoa elimu ya usimamizi na uendeshaji wa vikundi vya kiuchumi ikiwemo masuala ya ujasiriamali,usimamizi wa fedha,utunzaji wa kumbukumbu na utaftahi wa masoko.
Meya wa Manispaa ya Geita Mhe. Constantine Morandi amesema Manispaa ya Geita inatambua kwa kuona thamani ya Wananchi na wameongeza bidii ya makusanyo na kutenga zaidi ya bilioni moja ambapo katika kuelekea kuadhimisha miaka yao mitano wanajivunia kuwa sehemu ya mafanikio.
Vikundi 100 vyenye wanachama 503 kupitia uongozi wa samia tunanufaika na mikopo isiyo na riba huko mitaani kuna mikopo ya kausha damu huenda kuna wachache wamekutana nayo na shida za huko mnazijua lakini leo Serikali inawakopesha bila riba na ukirejesha kwa wakati una sifa ya kukopa tena na waitumie mikopo kwa malengo yaliyokusudiwa.
Katibu Tawala Wilaya ya Geita Bi. Lucy Beda amesema wanaptata leo Mkopo wamepitia mchakato wote na kukidhi vigezo na vikundi vyote vimepita kwenye kamati ya uhakiki na tumevitembelea na wako vizuri na wale ambao hawajakidhi masharti basi wafatilie kujua wapi walikwama na kujipanga upya.
Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe. Hashim Komba ameipongeza Manispaa ya Geita kwa kutekeleza vema utoaji wa mikopo kwa kiasi kikubwa mikopo ambayo inatoa fursa ya kuwawezesha wajasiriamali kiuchumi waweze kuendesha maisha yao.
Mikopo hii ni maono ya Mhe shimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kujenga Wananachi watakaoweza kujitegemea katika maisha yao na wahakikishe wanajijenga kiuchumi na wakikopeshwa zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa.
Aidha ameitaka Manispaa kwa kikundi kitachofanya vizuri na kurejesha bila shida na kwa kwa uaminifu wawape mikopo zaidi ili wajiendeshe kwa tija na kuleta mabadiliko makubwa katika jamii na pia waje na miradi mikubwa ya kuajiri watu wengi zaidi ili fedha hizi ziwe sehemu ya kuongeza tija za ajira.
Nao wafaidika wa mikopo wameishukuru Serikali kwa kuwapa mikopo isiyo na riba na kuahidi kuitumia kwa malengo waliyokusudia.
MATUKIO MBALI MBALI KATIKA PICHA
TUFUATILIE KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII
Instagram
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa