Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi wa ngazi ya kata katika Jimbo la Geita Mjini wameanza rasmi mafunzo yao leo, tarehe 04 Agosti 2025, katika Ukumbi wa EPZ Bombambili ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
Mafunzo haya yanawahusisha washiriki 26, ambao wanapewa elimu ya kina juu ya majukumu yao, misingi ya kisheria ya uchaguzi, na miongozo ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi. Lengo kuu ni kuwajengea uwezo wa kutekeleza majukumu yao kwa weledi, uadilifu na uaminifu mkubwa.
Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Geita Mjini, Ndugu Samson Ndaro, ndiye aliyefungua mafunzo hayo rasmi. Katika hotuba yake, amesisitiza umuhimu wa wasimamizi kufahamu majukumu yao kama sehemu muhimu ya kulinda amani, haki na uwazi katika mchakato wa uchaguzi.
Aidha, wasimamizi hao waliapishwa kwa kula kiapo cha kutunza siri na kuacha uanachama wa vyama vya siasa ili kuhakikisha utendaji wao unazingatia maadili ya uchaguzi na kutokuwa na upendeleo.
Mafunzo haya ni sehemu ya mkakati wa kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa uwazi, haki na amani, huku kila msimamizi akitekeleza wajibu wake kwa kufuata sheria na miongozo ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.
TUFUATILIE KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII
Instagram
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa