KAMPUNI YA BLUE COAST INVESTMENT YATOA MADAWATI 200 KWA HALMASHAURI YA MJI GEITA
Halmashauri ya Mji Geita imepokea madawati 200 yenye thamani ya Shilingi Milioni 15 yaliyotolewa na Kampuni ya Blue Coast Investment ya Mjini Geita ikiwa ni mchango wake kwa jamii inayowazunguka.
Akikabidhi madawati hayo, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Ndg. Athanas Inyasi amesema kuwa ameguswa kutoa mchango huo kwa sababu yeye kama mzazi anajisikia uchungu kuona baadhi ya wanafunzi wanakaa chini wanapokuwa darasani hali itakayopelekea watoto hao kutoelewa masomo wanayofundishwa.
Ndg. Athanas Inyasi ameongeza kuwa mchango huo ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli kwa kuhakikisha wanafunzi wanajengewa mazingira rafiki ya sehemu ya kujifunzia.
Akipokea madawati hayo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Geita Mhandisi Modest Apolinary ameishukuru kampuni ya Blue Coast Investment kwa kutambua umuhimu wa wanafunzi kukaa kwenye madawati katika shule zote za msingi ndani ya Halmashauri ya Mji wa Geita. Madawati hayo yamepunguza kwa sehemu kubwa uhitaji wa madawati katika Halmashauri ya Mji Geita.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa