Machinjio Ya Kisasa Mpomvu Kuwainua Wananchi Kiuchumi
Ujenzi wa Machinjio ya kisasa Mpomvu katika Halmashauri ya Mji wa Geita ambao uko katika hatua za ukamilishaji utawanufaisha wananchi wa Geita na maeneo ya Jirani kwa kupata ajira mbalimbali ndani ya machinjio hayo, upatikanaji wa kitowewo na usafirishaji, Ngozi kwa ajili ya viwanda, mradi wa gesi kutokana na kinyesi cha ng’ombe nk.
Tathimini hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Rosemary Senyamule hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mheshimiwa Rosemary Senyamule wakati wa hafla ya kumpongeza Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuuwezesha Mkoa wa Geita kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya Shilingi Bilioni 416 za kitanzania.
Mhe. Senyamule pia amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuleta neema ya mradi mkubwa wa maji katika mji wa Geita na baadhi ya kata za Halmashauri ya Wilaya ya Geita, mradi ambao utamtua mama ndoo kichwani kwa kuondoa kabisa kero ya maji kwa wananchi wa mji wa Geita.
Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe. Wilson Shimo amesema kuwa ujenzi wa vyumba 415 vya madarasa katika wilaya yake ambavyo vimejengwa kwa fedha za UVIKO-19 umewezesha kupunguza kabisa msongamano wa wanafunzi mashuleni na kuwarahisishia walimu kazi ya kufundisha idadi ya wanafunzi katika uwiano unaotakiwa.
Mhe. Shimo amemshukuru mama Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuipatia wilaya ya Geita Zaidi ya shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami katika majimbo yote matatu ya uchaguzi ndani ya wilaya yake. Kadhalika amempongeza Rais kwa kufufua ujenzi wa chuo cha ufundi stadi VETA mjini Geita, ujenzi ambao ulikuwa umesimama kwa kipindi kirefu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita Bi. Zahara Michuzi ametoa shukrani za dhati kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupokea Zaidi ya shilingi Bilioni 10 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo ya barabara, zahanati na vituo vya afya, Shule mpya ya Sekondari kupitia mradi wa SEQUIP, mikopo kwa makundi maalum, fedha za TASAF, Vyumba vya madarasa na ujenzi wa uwanja wa michezo Geita mjini.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa