JUKWAA LA KUTANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI NA BIASHARA KUFANYIKA GEITA.
Wilaya ya Geita inatarajia kuwa mwenyeji wa Jukwaa la Kutangaza fursa za Uwekezaji na Biashara katika Mkoa wa Geita.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita kwa kushirikiana na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (Tanzania Standard Newspapers – TSN) inayochapisha magazeti ya Daily News, HabariLeo na SpotiLeo imeandaa Jukwaa la Fursa za Uwekezaji na Biashara litakalofanyika tarehe 16 Agosti 2018 kuanzia saa 2:00 asubuhi katika Ukumbi wa GEDECO.
Pamoja na mada kutoka kwa viongozi wa Serikali, Wadau wa Maendeleo, Vikundi na makampuni mbalimbali yaliyoalikwa, yatafanyika pia maonesho ya bidhaa na huduma zinazopatikana ama kuzalishwa na wadau wa nje na ndani ya Mkoa. Maonesho haya yataanza kuanzia tarehe 14 hadi 16 Agosti, 2018 katika viwanja vya Ofisi ya Mkurugenzi wa Mji Geita.
Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Geita inawaalika wananchi wote wa Mji wa Geita na maeneo ya jirani kushiriki katika Jukwaa hili litakalotangaza fursa za uwekezaji katika Sekta mbalimbali zikiwemo madini, kilimo, ufungaji,huduma, uongezaji thamani n.k. Karibu Geita, karibu kwenye Jukwaa la fursa za Uwekezaji na Biashara.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa