Wataalamu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Geita leo tarehe 21 Julai 2025 wakiongozwa na Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Ndugu Robert Sungura, wametembelea na kukagua miradi ya TASAF ikiwa ni pamoja na mradi wa ujenzi wa nyumba pacha ya watumishi iliyopo katika kata ya Nyanguku, kijiji cha Mwagimagi. Mradi huo una thamani ya Shilingi 92,410,713.29 na umekamilika kwa asilimia 99.
Pia wametembelea mradi wa ujenzi wa jengo la huduma za nje (OPD) katika kijiji cha Mwagimagi, kata ya Nyanguku, mradi unaotegemewa kutumia kiasi cha Shilingi 92,410,714.29. Mradi huu umetekelezwa kwa asilimia 75 hadi sasa.
Wataalamu hao pia wamekagua ujenzi wa mabweni mawili yanayo simamiwa na Mitaa ya Shilabela na Moringe katika shule ya Sekondari Kalangalala, mradi wenye thamani ya Shilingi 305,579,549.91.
Timu hiyo imepongeza hatua Zinazofanywa na TASAF katika kuendeleza miradi ya maendeleo.
Akizungumza katika ziara hiyo, Ndugu Robert Sungura amesisitiza umuhimu wa mafundi kusimamiwa vizuri ili kuhakikisha miradi inakamilika kwa ubora unaotakiwa.
Naye Mratibu wa TASAF, Ndugu Amani Madenge, amesema TASAF itaendelea kusimamia miradi yote kwa ukamilifu na kuhakikisha inatekelezwa kwa ubora na kukamilika kwa wakati katika Manispaa ya Geita.
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA
TUFUATILIE KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII
Instagram
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa