Watumishi wa Halmashauri ya Mji Geita watakiwa kuchukua tahadhari na kujikinga na maambukizi ya virusi vya UKIMWI.
Hayo yamebainishwa leo tarehe 01 Disemba 2021 katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani yaliyofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji Geita yaliyohusisha Watumishi wa Halmashauri ya Mji Geita na wadau mbalimbali kama wawezeshaji.
Akifungua maadhimisho hayo Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Geita ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Bw. Lee Joshua aliwasihi watumishi kutokufanya ngono zembe mfano kufanya ngono pasipo matumizi ya kinga na ameshauri watumishi kupima afya zao mara kwa mara.
Akiongelea kuhusiana na maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa kufanya ngono zembe Bi. Amina Nghombo ambaye ni muwezeshaji kutoka Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Geita amesema mambo yanayoweza kusababisha maambukizi ya Virusi vya UKIMWI ni pamoja na unywaji wa pombe (unapoteza kumbukumbu na kufanya mtu kushindwa kujizuia kutokana na kilevi kilichomo).
Pia Bi. Amina ameelezea kuwa kufanya tohara (kutahiri) kunasaidia kupunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI.
Tume ya kuthibiti UKIMWI Tanzania (TUCAIDS) inaratibu maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani, ambayo hufanyika kila mwaka Disemba Mosi.
Madhumuni ya maadhimisho haya ni kutathmini hali na mwelekeo wa udhibiti UKIMWI Kitaifa na Kimataifa. Aidha, siku hii hutumika kuhamasisha na kuelimisha Jamii juu ya namna ya kujikinga na maambukizi mapya ya VVu, matumizi sahihi ya ARV kwa watu wanaoishi na VVu pamoja na kupinga unyanyapaa na ubaguzi.
Kauli mbiu ya maadhimisho haya ya mwaka huu ni ”ZINGATIA USAWA TOKOMEZA UKIMWI, TOKOMEZA MAGONJWA YA MLIPUKO”
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa