Leo tarehe 31 Januari, 2025 Halmashauri ya Manispaa ya Geita imefanya madhimisho ya siku ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele. Maadhimisho hayo yamefanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Uwanja iliyopo katika Kata ya Nyankumbu
Maadhimisho haya uadhinishwa tarehe 30 Januari kila mwaka ili kutilia mkazo udhibiti wa magonjwa haya pamoja na kuhamasisha jamii namna ya kujikinga na kupambana nayo.
Kauli mbiu ya mwaka huu inasema "Tuungane, Tuchukue hatua, Tutokomeze Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele." Maadhimisho haya yanalenga kuhamasisha katika ngazi za Halmashauri na wadau katika ngazi zote kushiriki kikamilifu katika kuhamasisha na kuelimisha jamii.
Magonjwa hayo ambayo yanadhibitiwa na mpango wa kitaifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ni pamoja na kichocho, minyoo tumbo, trakoma, usubi, matende na mabusha. Magonjwa haya yamo ndani ya jamii hasa jamii masikini lakini hayakuwa yanapewa umuhimu stahili kama ilivyo kwa magonjwa mengine kama vile Malaria, UKIMWI na mengineyo
Mpango wa kitaifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ulianza mwaka 2008 baada ya mikakati mbalimbali inayotumika kudhibiti magonjwa haya kuingizwa kwenye mpango kabambe wa wizara ya afya.
Dhumuni kuu la mpango huu ni kupunguza maradhi yatokanayo na magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele nchini ili kufikisha kiwango ambacho si tatizo katika jamii na mwaka 2012 Wizara ya Afya ilizindua mpango mkakati kwa ajili ya kudhibiti magonjwa haya.
Halmashauri ya Manispaa ya Geita imekuwa ikitekeleza shughuli mbalimbali dhidi ya kukabiliana na magonjwa ambayo yalikuwa hayapewi kipaumbele kama vile; kutoa dawa za kinga tiba kwa watoto wote wenye umri wa kwenda shule, kutoa elimu kwenye jamii na ujezi wa vyoo. Inakadiriwa watu zaidi ya bilion moja duniani kote tayar wameathirika na watu zaidi ya bilioni mbili walikuwa kwenye hatari ya kupata maambukizi ya magonjwa hayo.
Kwa kipindi cha mwaka 2024, Halmashauri ya Manispaa ya Geita ilikuwa na jumla ya walengwa 128,974 wenye umri wa kuanzia miaka 5 hadi 14 waliokuwa wameandikishwa shuleni na Halmashauri ilifanikiwa kutoa dawa za kinga tiba za minyoo tumbo kwa shule 97 za msingi na shule 32 za sekondari ambapo jumla ya wanafunzi 127,078 walimeza dawa za minyoo tumbo sawa na 98.52% ya walengwa wote na wanafunzi waliomeza dawa za kinga tiba za kichocho 84,604 ambao ni sawa na 96.53% ya walengwa 87,645 wote kutoka kwenye Kata ambazo zina maambukizi makubwa ya kichocho
Dkt. Sunday Mwakyusa, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ambaye ni mgeni rasmi amesema kuwa mikakati iliyopo ni kuhakikisha kuwafikia walengwa zaidi ya 100%
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Geita Dkt. Sunday Mwakyusa akizungumza jambo katika maadhimisho hayo
Maadhimisho haya yamehudhuriwa na maafisa mbalimbali kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Geita pamoja na Walimu na viongozi wa Kata na Mitaa, ambapo burudani mbalimbali zilitolewa pamoja na zoezi la utoaji wa dawa za kinga tiba za minyoo tumbo
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Geita Dkt. Sunday Mwakyusa akifafanua jambo katika maadhimisho hayo
Afisa Elimu Vifaa na Takwimu Shule za Msingi katika Manispaa ya Geita Ndg. Kapela Kahamba akiwa katika maadhimisho hayo
Afisa Lishe wa Manispaa ya Geita Ndg. Matovu Muhihi akitoa elimu ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele katika maadhimisho hayo
Afisa Elimu Watu Wazima katika Manispaa ya Geita Bi. Rahel Mwera akifafanua jambo katika maadhimisho hayo
Mmoja wa wanafunzi kutoka Shule ya Msingi Uwanja akipata dawa tiba kinga ya Minyoo tumbo katika maadhimisho hayo
Afisa Elimu Kata ya Nyankumbu Ndg. James Magela akifuatilia maadhimisho hayo
Mratibu wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele (NTD) Bi. Masau Fulano akifuatilia maadhimisho hayo
Baadhi ya Wanafunzi wakifuatilia maadhimisho ya siku ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele
Baadhi ya Wanafunzi wakifuatilia maadhimisho ya siku ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele
Wanafunzi wakitoa burudani katika maadhimisho ya siku ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele
Wanafunzi wakifurahia kupata elimu na vidonge vya tiba kinga ya minyoo ya tumbo katika maadhimisho ya siku ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa