• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Geita Town Council
Geita Town Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Geita

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Rasilimali Watu na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na Takwimu
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii,Ustawi wa Jamii na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Usafishaji
    • Vitengo
      • Uchaguzi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • Nyuki na Misitu
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uchimbaji Madini
    • Sekta ya Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Elimu na Afya
      • Kamati ya Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu ya Maombi
    • Miongozo
    • Jarida la Halmashauri
    • Mkakati wa kuziwezesha
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Kutotumia Dawa Ni Kujichimbia Kaburi - Mhe. Kanyasu

Posted on: December 2nd, 2022

Kutotumia Dawa ni Kujichimbia Kaburi – Mhe. Kanyasu

Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Mheshimiwa Costantine Kanyasu amewaasa watu wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kuendelea kutumia dawa zinazotolewa kwa ajili ya kufubaza makali ya virusi hivyo.

Mhe. Kanyasu ameyasema hayo Disemba mosi 2022 alipokuwa akizungumza na hadhira iliyokuwa imeshiriki maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika kiwilaya katika ukumbi wa shule ya Sekondari Shantamine kata ya Mtakuja.

Mbunge Kanyasu amewataka WAVIU kutoona aibu kufuata dawa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya au kutomeza dawa kutokana na maelekezo ya waganga wa tiba asilia na viongozi wa kidini ambayo yanawaaminisha katika uponyaji wa ugonjwa walionao kwa njia ya maombezi.

“Napenda kuwatahadharisha ndugu zangu WAVIU kutopuuzia matumizi ya dawa za kufubaza makali ya VVU au kutofuata kanuni za matumizi bora ya dawa pamoja na ushauri nasaha kutoka kwa wataalam wa afya, mkifanya hivyo mtakuwa mnafupisha muda wa Maisha yenu hapa duniani kwa makusudi.” Aliongeza Mhe. Kanyasu.

Mbunge wa Geita Mjini ameahidi kuwa ataendelea kushirikiana na Halmashauri yake katika kuhakikisha elimu juu ya kujikinga na maambukizi mapya ya VVU inaendelea kutolewa katika jamii ili kufanikisha malengo ya kuondoa maambukizi mapya, vifo vitokanavyo na ugonjwa wa UKIMWI na kuondoa tatizo la unyanyapaa kwa WAVIU ifikapo mwaka 2030. Kadhalika amewakumbusha wazazi na walezi kutochoka kuzungumza na Watoto pamoja na vijana wao juu ya kuepukana na matendo maovu ambayo yanakinzana na desturi za kitanzania pia yanachochea maambukizi ya Virusi vya UKIMWI.

Kwa upande wa Mwenyakiti wa Halmashauri ya Mji Geita Mhe. Costantine Morandi amesema kuwa kila mwananchi kwa nafasi yake achukue hatua za Madhubuti kuhakikisha anapambana na kutokomeza maambukizi mapya ya VVU kwani takwimu zinaonyesha kiwango cha maambukizi katika mji wa Geita bado ni kikubwa.

Akizungumza kwa niaba ya jumuiya ya watu wanaoishi na maambukizi ya VVU wilayani Geita kwa kifupi KONGA, Ndugu Ponsian Magezi ameiomba jamii kubadili tabia kama ulevi wa kupindukia, mila za kurithi wajane, biashara za ngono ambazo jamii imezikumbatia pasipo kutambua kuwa ni hatarishi na zinachochea kasi ya maambukizi ya VVU kuongezeka.

Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani kwa mwaka 2022 yalibeba kauli mbiu inayosema “IMARISHA USAWA” ambayo inasisitiza usawa katika maeneo yote ya utoaji wa huduma kwa kuzingatia usaa wa makundi yote pasipo kunyanyapaa hata mtu mmoja.


Matangazo

  • TANGAZO LA URASIMISHAJI WA MAKAZI YASIYOPANGWA January 16, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI July 22, 2022
  • TANGAZO LA KAZI ZA MACHINJIO August 16, 2022
  • MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA GEITA MJI December 02, 2022
  • Zaidi

Habari Mpya

  • Kamati Ya Siasa Wilaya Ya Geita Yaridhishwa na Miradi Geita Mji

    January 26, 2023
  • Walimu 668 Geita Mji Wanufaika na Vishikwambi

    January 18, 2023
  • Wanufaika Washauriwa Kuanzisha Viwanda Vidogo

    December 27, 2022
  • Timu Ya Halmashauri Yapata Udhamini Kutoka GGM

    December 20, 2022
  • Zaidi

Video

Machinjio ya Kisasa Mpomvu Yaanza kazi
More Videos

Kurasa za Karibu

  • Applications Forms
  • Acts
  • Barua pepe za watumishi
  • Taarifa za Huduma za Afya
  • Wasiliana nasi
  • Malalamiko
  • Taarifa za Mapato

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Geita Tanzania

    Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita

    Namba ya Simu: 0282520437

    Mobile:

    Barua pepe: td@geitatc.go.tz

Mawasiliano Zaidi

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa