KIKUNDI CHA BAGOLO KUJIKWAMUA KIUCHUMI KWA UFUGAJI
Vijana watano walioko katika kikundi cha Bagolo, kijiji cha Nyambogo kata ya Shiloleli, Halmashauri ya Mji Geita ambao wamepata mkopo wa Shilingi Milioni kumi na tano (15,000,000) kama mkopo kwa vikundi vya wanawake na vijana wamejiwekea malengo ya kujikwamua kiuchumi kutoka katika fedha hiyo.
Vijana hao wamenunua ng’ombe 10 ambao ni madume ya kunenepesha, ng’ombe hao watafugwa kwa muda wa miezi 3 hadi 5 na kuwauza kwa ajili ya nyama ambapo ng’ombe mmoja atauzwa kati ya shilingi laki tisa hadi milioni moja.
Akizungumza wakati wa ziara ya wataalam wa Idara ya Maendeleo walipotembea kukagua shughuli zao Mwenyekiti wa kikundi hicho Ndg. John B. Fulana amesema waliamua kufanya shughuli ya ufugaji wa kunenepesha ng’ombe kwa sababu biashara hiyo inazalisha faida kubwa tofauti na ng’ombe wa maziwa, pia ufugaji wao ni rahisi kulingana na mazingira waliyonayo katika kijiji chao.
Ndg. Fulani amesema kuwa licha ya ufugaji ng’ombe kikundi chake kinajishughulisha na kazi nyingine kama ujenzi wa nyumba bora za kuishi na majengo ya shule, zahanati nk, kijijini kwao. Pia wamejipanga kulima mahindi, mpunga na pamba katika mashamba yao binafsi.
Mhasibu wa Kikundi hicho Bw. Sixbert A. Kakombola amesema kuwa kikundi chake kinategemea kurudisha marejesho baada ya miezi mitatu tangu walipokopeshwa na deni lote litakamilishwa baaada ya mwaka mmoja.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa