Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe Mohamed O. Mchengerwa(Mb) Leo Mei 23, 2025 amefungua Kikao Kazi cha Maafisa Habari wa Mikoa, Halmashauri na Taasisi za Ofisi ya Rais TAMISEMI katika Ukumbi wa Mikutano DodomaJiji ulipo Mji wa Serikali Mtumba.
Katika Kikao Kazi hicho Mhe Mchengerwa amewataka Maafisa Habari Nchini kutoa taarifa sahihi ya yale yanaoyoendelea kwenye maeneo yao.
" Ninyi ni nguzo ya maamuzi ya kuwalisha watanzania ya kile kinachoendelea katika maeneo yenu" Amesema Mhe Mchengerwa (Mb)
Pamoja na hayo Mhe Mchengerwa amewataka Maafisa Habari kuweka Uzalendo mbele katika kuisemea miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa katika maeneo yao.
Kikao hicho kitaendelea kwa siku mbili ambapo Maafisa Habari kote Nchini wamekutana kuendelea kubadilishana uzoefu namna bora ya kuzitangaza kazi za Serikali katika maeneo yao.
Miongoni mwa Halmashauri zilizoshiriki Kikao Kazi hicho kutoka Mkoa wa Geita ni pamoja na Halmashauri ya Manispaa ya Geita, Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Chato, Nyang'wale na Mbogwe.
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA
TUFUATILIE KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII
Instagram
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa