Idara ya Afya kupitia kitengo cha huduma za lishe kinaendelea kutekeleza shughuli zote zilizopo kwenye mkataba wa lishe na kuboresha huduma za afya kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya lishe bora kwa watoto chini ya umri wamiaka mitano (5).
Katika kuhakikisha lengo linafikiwa, Kitengo cha huduma za Lishe kimeweka malengo mathubuti kama, kufanya ukaguzi wa chakula, kufanya ukaguzi na usimamizi shirikishi vituoni, utekelezaji wa mpango wa upatikanaji wa chakula mashuleni, elimu ya lishe kwa wajawazito, kufanya upimaji wa hali ya lishe kwa watoto chini ya miaka mitano na kutoa matibabu ya utapiamlo, kuhamasisha matumizi ya unga wa virutubisho shuleni, na kuongeza utoaji wa nyongeza ya matone ya vitamini A na dawa za minyoo kwa Watoto wa umri chini ya miaka mitano (5).
Hata hivyo Kitengo cha Huduma za Lishe kimepata mafanikio mengi katika kipindi cha robo ya Aprili hadi Juni 2024.
Kwanza, Kufanya na kushiriki maadhimisho ya siku ya Afya na lishe katika kata za Buhalahala, Nyankumbu, Kalangalala na Kasamwa, ambapo elimu ya Lishe ilitolewa kwa kuonesha makundi ya vyakula, kufanya jiko darasa na kupima hali ya lishe kwa Watu wote.
Kushiriki katika mwezi wa Afya na lishe na kufanya uzinduzi wa kampeni ya utoaji wa nyongeza ya matone ya vitamini A ambapo katika kampeni hiyo waliweza kufikia jumla ya Watoto 66,574 sawa na asilimia 119.5.
Pia Kitengo cha Huduma za Lishe kimeshiriki katika maadhimisho na mikutano mbalimbali katika kada za Afya, Elimu na Dini, kama madhimisho ya wiki ya elimu, siku ya Mtoto wa Afrika na mikutano ya dini.
Aidha katika mwaka wa fedha 2024/25, Kitengo cha Huduma za Lishe kimepanga kununua vibao 12 vya kupimia urefu ili kutatua changamoto ya vipimo pamoja na kuendelea kuhamasisha na kushirikisha wadau mbalimbali kuhusu umuhimu wa lishe kwa kwa Watoto.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa