Mkuu wa Idara ya Kilimo, Uvuvi na Ufugaji wa Manispaa ya Geita, Ndugu Leonard chacha, ameendelea kutoa elimu na maarifa muhimu kwa wananchi wanaotembelea banda la Manispaa katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Nyamhongolo, jijini Mwanza.
Ndugu chacha amekuwa akielimisha wakulima, wafugaji na wavuvi juu ya:
- Mbinu bora za kilimo chenye tija
- Ufugaji wa kisasa wenye lengo la kuongeza kipato
- Teknolojia rahisi za uvuvi endelevu
- Lishe bora ya mifugo na usimamizi wa magonjwa.
Wananchi wanaendelea kufurika kwa wingi katika banda hilo, wakijifunza kwa vitendo na kupata ushauri wa moja kwa moja kutoka kwa wataalamu waliopo.
TUFUATILIE KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII
Instagram
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa