Kamati ya Siasa Wilaya Yakoshwa na Ubora wa Miradi
Wajumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Geita ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Geita Barnabas Mapande wameridhishwa na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika Halmashauri ya Mji Geita.
Akizungumza wakati wa ziara ya Kamati hiyo kukagua utekelezaji wa Ilani hivi karibuni, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Geita ameishukuru Serikali ya Awamu ya sita chini ya jemedari Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuipatia fedha Halmashauri ya Mji Geita, fedha ambazo zimetekeleza na zinaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
“Mama Samia Suluhu Hassan ana dhamira ya dhati katika kuhakikisha watanzania wanapata huduma muhimu za msingi katika Zahanati zenye viwango, shule bora za Msingi na Sekondari, Hudumay a maji safi na salama Pamoja na Barabara zinazopitika wakati wote. Hivyo wasimamizi kwa ngazi ya Halmashauri msaidieni Mhe. Rais ili nia yake iweze kutekelezeka kikamilifu na kwa usahihi kwa sababu mmepokea fedha nyingi ili kujenga miradi yenye “. Aliongeza Mhe. Mapande.
Wajumbe wa Kamati ya Siasa wamefurahishwa na maboresho ya elimu ya awali yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya sita kupitia mradi wa uboreshaji wa Elimu ya Awali na Msingi(BOOST) ambapo katika Halmashauri ya Mji Geita madarasa ya awali ya mfano yamejengwa kisasa na kuwekewa mabembea ya kuchezea kwa lengo la kumfanya mtoto apende Kwenda shule, jambo ambalo kwa miaka ya nyuma lilikuwa likifanyika katika shule za watu binafsi na zile za taasisi za kidini pekee.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM Wilaya ya Geita Bi. Naomi Fujo amewaasa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ambao wameanzisha vikundi vinavyojishughulisha na Kazi mbalimbali za kujiingizia kipato kutokuwa waoga kukopa kwenye taasisi za kifedha ambazo zinatoa mikopo yenye riba nafuu, bali wanatakiwa watumie fursa hizo ili kukuza mitaji yao na kujiongezea kipato kikubwa zaidi ya kile walichonacho.
Miradi iliyotembelewa na Kamati ya Siasa Wilaya ya Geita ni Pamoja na Ujenzi wa mabweni mawili ya wanafunzi katika Shule ya Sekondari Geita, ujenzi wa Zahanati ya Kigoma road, Kikundi cha wanawake cha kukamua mafuta ya alizeti Kanyala, Shule mpya ya Msingi Chanama, Shule mpya ya Msingi Juhudi na ujenzi wa Barabara za mitaa katika Kata za Kanyala na Bombambili.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa