Kamati ya LAAC Yaridhishwa na Miradi Geita Mji
Halmashauri ya Mji Geita imepongezwa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kujiridhisha kuwa miradi hiyo ina ubora unaotakiwa kwa manufaa ya wananchi.
Wajumbe wa Kamati hiyo wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti Mheshimiwa Stanslaus Mabula (Mb) hivi karibuni wamefanya ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo imetekelezwa na inaendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Mji wa Geita.
Kamati ya LAAC imetoa pongezi kwa Madiwani pamoja na wataalam kwa kubuni wazo zuri la kuanzisha mradi wa uwanja wa michezo Geita mjini ambacho kitakuwa ni chanzo kikubwa cha mapato ya Serikali na pia kitatoa fursa kwa wananchi wa Geita kutazama mashindano mbalimbali ya michezo katika uwanja wa nyumbani.
Wajumbe wa Kamati hiyo wametoa agizo kwa Halmashauri ya Mji Geita kuhkikisha ujenzi wa uwanja huo unakamilika ifikapo mwishoni mwa mwezi Januari 2025 na kuanza kutumika katika mashindano mbalimbali ya michezo kuanzia ngazi ya Wilaya, Mkoa, Taifa hadi kimataifa.
Akizungumza kwa niaba ya wajumbe wengine Mhe. Stanslaus Mabula (Mb) amewashauri wataalam wote kutunza jengo la ofisi na miundombinu yake ili kuendelea kulitunza jengo hilo ambalo kuwa limejengwa kwa kiwango chenye ubora wa hali ya juu na linatoa taswira nzuri ya Mji wa Geita.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita Mhe. Costantine Morandi ametoa shukrani za dhati kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuiwezesha Halmashauri yake kupata vituo vinne vya afya ndani ya kipindi cha uongozi wake tofauti na miaka ya nyuma ambapo Halmashauri ilikuwa na kituo cha Afya kimoja pekee.
Miradi iliyotembelewa na Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa ni pamoja na ujenzi wa Uwanja wa michezo Geita mjini, upanuzi wa Kituo cha Afya Bulela pamoja na ukaguzi wa jengo la Ofisi kuu ya Halmashauri ya Mji Geita katika eneo la Magogo.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa