Kamati ya Lishe ya Halmashauri ya Manispaa ya Geita imefanya ziara ya Ufuatiliaji wa Huduma za Lishe Shuleni ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuhakikisha utekelezaji wa mpango wa chakula mashuleni unakwenda sambamba na maboresho ya afya na ustawi wa wanafunzi.
Lengo kuu la ziara hii ni kufanya usimamizi shirikishi wa masuala ya lishe kupitia maeneo yafuatayo:
- Utekelezaji wa mpango wa chakula mashuleni
- Uhamasishaji wa matumizi ya unga wa mahindi ulioboreshwa kwa virutubishi
- Uanzishaji wa klabu za lishe
- Uanzishaji wa bustani za mboga mashuleni
Kupitia hatua hizi, Kamati inalenga kuboresha afya na lishe za wanafunzi, kupunguza hali ya udumavu na utapiamlo, kuimarisha mahudhurio, kuongeza ufaulu, na kujenga kizazi chenye afya bora.
Katika ziara hiyo, jumla ya shule 10 zilitembelewa (tano za msingi na tano za sekondari shule) zote zinaendesha mpango wa chakula mashuleni na kuhakikisha wanafunzi wanapata angalau mlo mmoja wakiwa shuleni. Aidha, Kamati imefurahishwa na hali ya utekelezaji wa mpango wa chakula, uwepo wa klabu za lishe pamoja na bustani za mboga ambazo zimeanza kuonekana kama chanzo muhimu cha lishe mbadala.
Kamati inaendelea kutoa elimu ya lishe kwa jamii na mashuleni ili kuongeza uelewa na kuhamasisha ushiriki wa wazazi katika uchangiaji wa chakula mashuleni, kwa manufaa ya afya na maendeleo ya watoto.
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA
TUFUATILIE KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII
Instagram
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa