Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita na Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Uongozi ambaye pia ni Mheshimiwa Diwani wa Kata ya Mtakuja Mhe. Costantine Morandi Mtani leo tarehe 03 Februari, 2025 ameongoza wajumbe wa kamati ya fedhana uongozi kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Geita.
Kamati ya fedha na uongozi wakikagua ujenzi wa Daraja katika Kata ya Shiloleli
Kamati hiyo ikijumuisha baadhi ya Waheshimiwa na Wakuu wa Idara na Vitengo wametembelea na kukagua ujenzi wa Daraja katika Kata ya Shiloleli, ukamilishaji wa chumba cha darasa katika shule ya Msingi Gamashi iliyopo Kata ya Bulela, ukamilishaji wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) katika Zahanati ya Gamashi iliyopo Kata ya Bulela, kutembelea na kukagua ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) na nyumba ya Mganga wa Zahanati (2 in 1) katika Zahanati ya Mwagimagi iliyopo katika Kata ya Nyanguku na kutembelea na kukagua mradi wa uzalishaji wa tofari unaomilikiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Geita.
Kamati ya fedha na uongozi wakikagua ukamilishaji wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) katika Zahanati ya Gamashi iliyopo Kata ya Bulela
Kamati ya fedha na uongozi wakikagua ukamilishaji wa chumba cha darasa katika shule ya Msingi Gamashi iliyopo Kata Bulela
Wajumbe wa Kamati ya Fedha na Uongozi walipongeza wasimamizi wa miradi kwa usimamizi wao mzuri na waliagiza uongozi wa Halmashauri Manispaa kuongeza usimamizi wa karibu kwa miradi yote ya maendeleo kupitia wataalam wake mbalimbali.
Nyumba ya Mganga wa Zahanati (2 in 1) katika Zahanati ya Mwagimagi iliyopo katika Kata ya Nyanguku
Kamati ya fedha na uongozi wakikagua ujenzi jengo la nyumba ya Mganga wa Zahanati (2 in 1) katika Zahanati ya Mwagimagi
Ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) katika Zahanati ya Mwagimagi iliyopo katika Kata ya Nyanguku ukiwa katika hatua ya msingi
Mradi wa uzalishaji wa tofari unaomilikiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Geita
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa