Pongezi hizo zimetolewa leo tarehe 05 Mei, 2025 na Waheshimiwa Madiwani ambao ni wajumbe wa Kamati ya fedha na uongozi wakati wa ziara ya Kamati ya fedha na uongozi kwa robo ya tatu kwa mwaka wa fedha 2024/2025 walipotembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Geita.
Wahe. Madiwani wamepongeza sana juhudi za Mkurugenzi wa Manispaa ya Geita Ndg. Yefred Myenzi na Menejimeti nzima ya Manispaa hii na wamesisitiza Mkurungezi na timu yake kuendelea kusimamia vyema miradi na kuendelea kuibua miradi ya kukusanya mapatao kama alivyofanya katika soko la Nyankumbu
Naye Ndg. Myenzi ameahidi miradi viporo ya CSR iliyopo katika baadhi ya Kata katika Halmashauri ya Manispaa ya Geita inatarajiwa kukamilishwa ndani ya wiki tatu (3) zijazo.
Na ameendelea kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa pesa nyingi za miradi anazoleta na kuahidi kuzisimamia vyema ili zilete tija kwa wananchi na jamii kawa ujumla
Kamati ya fedha na Uongozi ikiongzwa na Mhe. Elias Ngole ambaye ni Diwani wa Kata ya Nyanguku aliambatana na wajumbe mbalimbali wakiwemo Wahe. Madiwani, Mkurugenzi wa Halmashauri na Wataalamu wa kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Geita
Ziara hiyo iliweza kutembela miradi ya maendeleo ifuatayo; Kutembelea na kukagua marekebisho ya milango ya Zahanati ya Gamashi iliyopo katika Kata ya Bulela, kutembelea na kukagua ujenzi wa vibanda katika soko la Nyankumbu lililopo Kata ya Nyankumbu, kutembelea na kukagua ukamilishaji wa jengo la maabara katika shule ya sekondari Bombambili (CSR) iliyopo katika Kata ya Bombambili
Miradi mingine iliyoweza kufikiwa ni pamoja na kutembelea na kukagua ukamilishaji wa Zahanati ya Bombambili iliyopo katika Kata ya Bombambili, kutembelea na kukagua ukamilishaji wa jengo la utawala katika shule ya sekondari Kisesa (CSR) iliyopo katika Kata ya Buhalahala na kutembelea na kukagua ukamilishaji wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) na nyumba ya mtumishi katika Zahanati ya Mwatulole iliyopo katika Kata ya Buhalahala.
TUFUATILIE KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII
Instagram
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa