Kamati ya Bunge Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ikiongozwa na Mwenyekiti ambaye ni Mbunge wa jimbo la Kilolo Mkoani Iringa Mhe. Justine Nyamoga imefanya ziara ya kukagua ujenzi wa Barabara ya Kasco- Uhamiaji ,Ujenzi wa shule maalum ya Sekondari ya wasichana Geita tarehe 16 Machi 2025 katika Manispaa ya Geita. Wakiwa katika ziara yao, wajumbe hao wametoa pongezi za dhati kwa viongozi wa Manispaa ya Geita kwa usimamizi bora wa miradi miwili waliyoitembelea.
Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe.Hashim Komba amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za utekelezaji wa Miradi ya maendeleo na kufanikisha ujenzi wa Shule za Sekondari za kisasa katika Kata zote 50 za Wilaya ya Geita.
Akishukuru kwa niaba ya Manispaa, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Geita Mhe. Costantine Morandi ametoa shukrani kwa Serikali ya awamu ya sita
kwa kuendelea kuipatia Manispaa ya Geita fedha nyingi za ujenzi wa Barabara za Mitaa pamoja na Miradi mingine ya maendeleo.
Wajumbe wa Kamati hiyo pia wamempongeza Diwani wa Kata ya Bombambili Mhe. Leonard Bugomola kwa namna alivyoshirikiana na wananchi pamoja na viongozi wa Kata yake kuhakikisha ujenzi wa Shule ya maalum ya Sayansi ya Wasichana unafanikiwa kwa asilimia 100%
Pia ameishukuru Kamati hiyo kwa kutembelea na kukagua utekelezaji wa Miradi ya maendeleo katika Manispaa ya Geita
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa