Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita Ndg. Sostenes Mbwilo leo tarehe 17 Aprili, 2025 amefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa kupitia wajibu wa kampuni kwa jamii (Corporate Social Responsibility - CSR) katika Halmashauri ya Manispaa ya Geita.
Katika ziara hiyo, Kaimu Mkurugenzi aliambatana na Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi wa Halmsahauri Ndg. Mhina, Kaimu Mhandisi Ndg. Josiah Salaa, Kaimu Mkuu Mkuu wa Idara ya Mipango na Ufuatiliaji Ndg. Egnus Domition, Mkadiriaji Majengo Bi. Doreen Mollel na Afisa Ugavi Josephat Gombeye.
Miradi kumi na moja (11) imeweza kufikiwa, kutembelewa na kukaguliwa na Kaimu Mkurugenzi pamoja na timu yake aliyoongozana nayo kama ifuatavyo;
Ametembelea na kukagua ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) katika zahanati ya Bombambili iliyopo katika kata ya Bombambili.
Ujenzi jengo la maabara katika shule ya Sekondari ya Bombambili iliyopo katika kata ya Bombambili na mradi huu upo hatua ya umaliziaji kwa kuweka mifumo ya “gas”
Ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) na ujenzi wa nyumba ya Mtumishi katika zahanati ya Buhalahala iliyopo katika Kata ya Buhalahala.
Ujenzi wa miradi hii ipo katika hatua mbalimbali za umaliziaji (finishing).
Ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari Kisesa Geita iliyopo katika Kata ya Kalangalala ambapo mradi huu pia upo katika hatua mbalimbali za ukamilishaji. Aidha amekagua mradi wa vyoo vya wanafunzi ambavyo tayari vilishakamilika na kuanza kutumika.
Ametembelea na kukagua ujenzi wa ukamilishaji wa jengo la maabara katika zahanati ya Nyakabale iliyopo katika Kata ya Mgusu ambapo mradi huu upo hatua za mwisho kwa ajili ya kuanza kutumika.
Ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari Mgusu iliyopo katika Kata ya Mgusu ambapo mradi huu upo katika hatua za ukamilishaji wa ufungaji wa milango.
Ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) katika zahanati ya Mgusu iliyopo katika Kata ya Mgusu. Ujenzi wa mradi huu upo katika hatua mbalimbali za ukamilishaji wa marekebisho madogo madogo na ambapo jengo hili tayari limeshaanza kutoa huduma kwa wananchi.
Ujenzi nyumba ya Mtumishi katika zahanati ya Mgusu iliyopo katika Kata ya Mgusu. Ujenzi wa miradi huu umekamilika na watumishi wanaishi.
Ukamilishaji wa majengo ya shule ya msingi Samina iliyopo katika Kata ya Mtakuja ambapo mradi huu upo hatua za mwisho na madarasa husika yameshaanza kutumika.
Kaimu Mkurugenzi alikamilisha ziara yake kwa kutembelea na kukagua ukamilishaji wa ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) na nyumba ya mtumishi katika zahanati ya Bwihegule iliyopo katika Kata ya Mtakuja.
pamoja na kuwapongeza wasimamizi wa miradi yote hiyo pia amewaagiza wasimamizi hao kuhakikisha wanawasimamia mafundi ili waweze kuongeza kasi katika kuhakikisha wanaikamilisha na kuikabidhi mapema miradi ambayo haijakamilika ili ianze kutoa huduma kama inavyotakiwa na katika viwango sahihi.
Aidha, Kaimu Mkurugenzi amesema anamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa fedha za maendeleo anazozileta Katika Halmashauri ya Manispaa ya Geita kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa