Mkurugenzi wa Manispaa ya Geita alifungua kikao kwa kuwapongeza watumishi wote kwa kufanikisha ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri kwa kiwango cha 100.23%, sawa na shilingi bilioni 19 kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Alibainisha kuwa siri ya mafanikio haya ni mshikamano na ushirikiano wa dhati kutoka ngazi ya mtaa hadi makao makuu.
Mkurugenzi ametoa wito kwa watumishi wote kuendelea kushikamana na kushirikiana katika kutekeleza bajeti ya mwaka mpya wa fedha 2025/2026 kwa kuzingatia Mpango Mkakati uliowekwa.
Alisisitiza kuwa kila idara ina jukumu la kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa makubaliano ya kikao hiki.
Mkurugenzi amesisitiza umuhimu wa kuoanisha thamani ya fedha na miradi inayotekelezwa kwa kuzingatia:
•Taratibu sahihi za manunuzi
•Ubora wa bidhaa na huduma
•Ufanisi katika matumizi ya muda
Watumishi wamehimizwa kujishughulisha na kazi halali za kuongeza kipato, kama vile kilimo na biashara za mazao, baada ya saa za kazi, kwa sharti la kutoathiri utendaji wao wa kazi za kiserikali.
Imesisitizwa kuwa utunzaji wa afya na kuepuka migogoro kazini na nyumbani ni msingi wa utendaji bora kazini na maisha kwa ujumla.
Katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, Mkurugenzi alikumbusha kuwa maandalizi yanaendelea vizuri. Watumishi walioteuliwa kwa dhamana mbalimbali ndani ya Tume Huru ya Uchaguzi wanatakiwa kuzingatia sheria, kanuni, na maadili ya kazi hiyo.
Pia alisisitiza kuwa ni marufuku kufanya siasa mahali pa kazi na kila Mtumishi ahakikishe anashiriki kupiga kura.
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA
TUFUATILIE KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII
Instagram
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa