• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Geita Town Council
Geita Town Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Geita

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Rasilimali Watu na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Afya, Ustawi wa jamii na Huduma ya Lishe
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Miundombinu, Maendeleo vijijini na Mjini
      • Usimamizi taka na Usafi wa Mazingira
    • Vitengo
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi Mazingira
      • Sheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Mawasiliano Serikalini
      • Usimamizi wa Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uchimbaji Madini
    • Sekta ya Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Afya, Ustawi wa jamii na Huduma ya Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Elimu na Afya
      • Kamati ya Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu ya Maombi
    • Miongozo
    • Jarida la Halmashauri
    • Mkakati wa kuziwezesha
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
  • Maeneo ya Uwekezaji

Geita Youth Group Wakabidhiwa Gari

Posted on: April 17th, 2020

GEITA YOUTH GROUP WAKABIDHIWA GARI

Kikundi cha vijana wa Geita Youth wamekabidhiwa rasmi lori aina ya FAW pamoja na mashine mbili za kufyatulia matofali kutoka Halmashauri ya Mji wa Geita Tarehe 15/4/2020 katika viwanja vya Halmashauri ya Mji wa Geita. Gari na mashine hizo vikiwa ni mali zilizonunuliwa kutoka kwenye fedha kiasi cha Shilingi 163,025,000/= zilizotolewa kama mkopo na Halmashauri ya Mji wa Geita mapema mwezi Machi 2020.

Akipokea gari hilo na kuzungumza kwa niaba ya wanakikundi wenzake, Mwenyekiti wa kikundi hicho Ndugu Gabriel Nyasilu ameshukuru uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Geita kwa kukubali andiko lao na kuwapatia kiasi kikubwa cha mkopo walioomba ili waweze kuendesha shughuli zao zitakazowakwamua kiuchumi.

Ndg. Nyasilu ameahidi kuwa wanakikundi wataenda kufanya kazi kwa bidi na weledi mkubwa  kama timu na hawahitaji kuingia katika dhambi ya kukwamisha vikundi vingine vya vijana kukosa mikopo kutoka Halmashauri endapo wao watashindwa kurejesha mkopo huo kama makubaliano baina yao na Halmashauri yalivyoainishwa.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita Mhe. Leonard Bugomola amewasihi vijana hao kuonyesha mfano wa kikundi bora na chenye dira kwa jamii ili vikundi vingine viige mfano kutoka kwao. Pia amewatahadharisha kutoharibu uaminifu uliojengwa kwao na Halmashauri ya Mji Geita kwa kutenda jambo lolote kinyume na makubaliano kwa sababu hali hiyo itavunja Imani ambayo jamii nzima imeijenga juu yao.

Kwa uande wake Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Geita Ndg. Mwinyiheri Baraza ameipongeza Halmashauri ya Mji Geita kwa kuwa Halmashauri ya Mji ya kwanza kutekeleza utoaji wa mkopo mkubwa kwa vikundi vya vijana, kadhalika amewataka vijana kuwaonyesha viongozi wa Geita Mji kuwa hawakufanya makosa kuwakopesha Milioni 163 bali mkawe chachu ya kuleta maendeleo katika jamii.

Diwani wa Kata ya Kasamwa Mhe. Mary Kasanda na Diwani wa Kata ya Kalangalala Mhe. Zephania Mahushi kwa pamoja wamewataka vijana hao kuungana, kushirikiana kikamilifu katika kutunza mali hiyo ili waweze kufanikisha malengo yao waliyojipangia na hatimaye waweze kurejesha fedha walizopatiwa na Halmashauri ya Mji wa Geita ambapo zitatumika kunufaisha vikundi vingine vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu vilivyo na mahitaji mbalimbali.



Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI WA MAOHOJIANO (ORAL INTERVIEW) KADA YA MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II September 27, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA MAHOJIANO MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II September 29, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 05, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KATIKA USAHILI September 21, 2024
  • Zaidi

Habari Mpya

  • SERIKALI YAONGEZA FEDHA ZA ELIMU BURE MANISPAA YA GEITA

    May 11, 2025
  • WASIOFANYA USAFI KATIKA MAENEO YAO KUCHUKULIWA HATUA - DC KOMBA

    May 10, 2025
  • MAFUNZO KWA VIKUNDI VINAVYOTARAJIWA KUPEWA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI

    May 09, 2025
  • BURIANI MHE DAVID CLEOPA MSUYA

    May 07, 2025
  • Zaidi

Video

WATENDAJI WA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA WATAKIWA KUTOJIHUSISHA NA ITIKADI ZA KISIASA
More Videos

Kurasa za Karibu

  • Mfumo wa Watumishi kujihudumia
  • Applications Forms
  • Acts
  • Taarifa za Huduma za Afya
  • Mfumo wa Kupata Leseni za Biashara ( Mfumo wa Tausi)
  • Barua pepe za watumishi
  • Wasiliana nasi
  • Malalamiko
  • Taarifa za Mapato

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • TUWE MFANO KWA TAIFA' Yefred Myenzi
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Geita Tanzania

    Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita

    Namba ya Simu: 0282520437

    Mobile:

    Barua pepe: td@geitatc.go.tz

Mawasiliano Zaidi

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa