Halmashauri ya Mji Geita imezindua upandaji miti kwenye kwenye maneo ya Ofisi ya Halmashauri ya Mji Geita leo tarehe 24.11.2021.
Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe. Wilson Simon Shimo ambaye ni mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo amepongeza juhudi za Halmashauri kwenye upandaji na utunzaji wa miti pamoja na utunzaji wa mazingira na kuagiza kuhakikisha miti iliyopanda inalindwa na kutunzwa ili iendelea kukua.
Aidha Mhe. Shimo amemwagiza Afisa Maliasili wa Halmashauri kusimamia sheria ili kuhakikisha misitu pamoja na vyanzo vya maji vinalindwa ipasavyo.
Afisa Maliasili wa Halmashauri hiyo Bw. Lee Joshua wakati akisoma taarifa fupi kwa mgeni rasmi amesema;
“Shughuli za upandaji miti unayoizindua leo tarehe 24.11.2021 inalenga kuupendezesha Mji wetu wa Geita ili uweze kuvutia kwa kuwepo kwa vivuli na kuboresha hali ya hewa katika Mji wetu. Lakini pia ni katika kutekeleza agizo la Mhe. Makamu wa Rais alilolitoa Mwezi Desemba, 2017 la kutaka kila Halmashauri kupanda miti milioni moja na laki tano (1,5000,000) kila mwaka”
“Ni imani yetu kwamba wakazi wengi katika Halmashauri ya Mji Geita wanao mwamko wa kupanda miti, hii inadhihirika wazi kwa kuona miti katika mashamba ya watu binafsi na katika maeneo yetu ya makazi, jambo ambalo limesababisha kupandwa kwa miti ipatayo laki saba na elfu ishirini (720,000) hadi kufikia leo kwa mwaka huu wa 2021/2022, na mingine mingine ikiendelea kupandwa kama tunavyoendelea leo” Alisema Bw. Lee
Siku ya upandaji miti kitaifa hufanyika kila mwaka ifikapo Aprili 1, ni siku ambayo sisi sote inatupasa kutekeleza wajibu wa kupanda miti ili kutunza mazingira na zaidi tukilenga umuhimu wa miti au misitu katika kupunguza matatizo ya mabadiliko ya tabia nchi, alifafanua Bw. Lee
Rai imetolewa kwa Wakazi wa Geita kutovamia misitu ya hifadhi iliyoko katika Halmasahuri ya Mji Geita kwani misitu tuliyonayo imevamiwa kwa shughuli mbalimbali kama vile kilimo, makazi, uchomaji wa mkaa, uchanaji wa mbao, ukataji wa nguzo zitumiwazo na wachimbaji wadogowadogo wa dhahabu, na kuchunga idadi kubwa ya mifugo hifadhini. Mambo haya kiujumla yanasababisha uharibifu mkubwa wa mazingira na hatimae kusababisha mabadiliko ya tabia nchi.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa