Halmashauri Ya Mji Geita Yanufaika na Vifaa Vya Michezo
Halmashauri ya Mji Geita imepokea vifaa vya michezo vyenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 6 kutoka Kampuni ya Isamilo Supplies Limited.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya kampuni yake hivi karibuni katika viwanja vya Makao makuu ya Halmashauri, Kaimu Meneja wa Kampuni ya Isamilo Ndugu Robison Mageta amesema kampuni yake imetoa vifaa mbalimbali vya michezo ikiwemo mipira na mahitaji ya wagonjwa katika Hospitali ya Mji Geita ikiwa ni Sehemu ya mchango wao kwa jamii inayowazunguka kupitia fedha za uwajibikaji kwa jamii (CSR).
Bw. Mageta ameongeza kuwa michezo ni afya, michezo ni ajira lakini pia michezo inaleta amani hivyo Kampuni ya Isamilo itaendelea kutoa kwa kadri ambavyo watazidi kupokea maombi ya mahitaji kutoka kwa makundi mbalimbali yaliyoko kwenye jamii.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Geita Bi. Zahara Michuzi ametoa shukrani kwa kampuni ya Isamilo kwa kuwakumbuka wagonjwa walioko katika Hospitali ya Mji pamoja na kina mama wajawazito. Kadhalika kwa kuendelea kukuza vipaji vya michezo kwa wanafunzi walioko shuleni kupitia vifaa mbalimbali vya michezo walivyovitoa.
“Naomba nitumie fursa hii kutoa rai kwa wadau, makampuni, Taasisi mbalimbali kujitokeza kwa wingi katika kutoa mahitaji kwa jamii inayowazunguka kama walivyoafanya Kampuni ya Isamilo”. Aliongeza Bi. Zahara Michuzi.
Kwa upande wake Afisa Michezo wa Halmashauri ya Mji Geita Bi. Juliana Kimaro amesema vifaa hivyo vya michezo vitasaidia kuinua sekta ya michezo ndani ya Halmashauri na kupun guza upungufu uliokuwepo katika baadhi ya shule.
Pamoja na vifaa hivyo vya michezo Kampuni ya Isamilo imetoa mashuka seti 50 pamoja na kitanda kimoja cha kujifungulia ambacho kitasaidia kukabiliana na vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa