GEITA MJI YAJIPIGA MSASA KUTOKA COSTECH
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Geita Bi. Zahara M. Michuzi ametembelea Banda la Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es salaam (TANTRADE) maarufu kama Sabasaba Jijini Dar es salaam Tanzania.
Akizungumza wakati wa ziara yake katika banda hilo hivi karibuni, Bi Zahara Michuzi amewashauri watanzania watembelee banda la COSTECH ili wajifunze vitu vingi vya kibunifu vinaoneshwa na wabunifu wa kitanzania kwa lengo la kutatua matatizo ya kijamii na kuiletea tija Serikali kwa kujipatia fedha za kigeni, kwa kuuza bidhaa zilizovumbuliwa na Watanzania wenzetu na kuisaidia Serikali isitumie fedha kununua bidhaa zinazozalishwa nchi nyingine.
Mkurugenzi Zahara alifafanua kuwa amejifunza baadhi ya maeneo ambayo atayafanyia kazi katika halmashauri yake ikiwa ni pamoja na ukusanyaji wa mapato, kusaidia matumizi sahihi ya rasilimali kama vile pikipiki za watendaji ili zisitumike kinyume na matarajio, mashine ya uchenjuaji dhahabu kwa wachimbaji wadogo na wakubwa pamoja na mashine ya kuzalishia kaboni kwa kutumia vifuu ambavyo vinapatikana hapa nchini.
Akihitimisha ziara hiyo fupi, Mkurugenzi Zahara alitoa rai kwa Viongozi wenzake kutembelea Banda la COSTECH lililopo mtaa wa SIDO waweze kujifunza na kutumia fursa ya kutumia bidhaa zinazopatikana katika banda hilo ambazo zinakidhi matumizi ya binadamu katika shughuli zake za kila siku.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa