Geita Mji Yajipanga kuepuka Mrundikano wa Wanafunzi
Kukamilika kwa ujenzi wa Shule tatu za Sekondari ambazo ni mpya na zinatarajiwa kukamilika kabla ya Fbruari 28/2021 kutawezesha wanafunzi kusoma kwa nafasi na kwa idadi inayokubalika ,hali itakayopelekea kupandisha pia kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi hao.
Hayo yamebainishwa na Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Mji wa Geita Mwalimu Rashid Muhaya wakati wa ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa shule hizo hivi karibuni.
Mwalimu Muhaya amefafanua kuwa ujenzi wa shule ya Sekondari Kisesa yenye madarasa matano utakapokamilika utawezesha baadhi ya wanafunzi kuhamishiwa kutoka shule ya Sekondari Kalangalala. Kadhalika kwa shule ya Sekondari Kisesa na Mkangara ambapo wanafunzi watahamishwa kutoka kwenye shule zilizoko jirani
Kulingana na takwimu zilizotolewa na idara ya elimu, wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari kwa kidato cha kwanza ni 1744, wavulanawakiwa ni 2823 na wasichana 2921. Wavulana 2256 na wasichana 2260 wamesharipoti na kuanza masomo ya kidato cha kwanza na kufanya idadi ya wanafunzi ambao wamesharipoti katika Halmashauri ya Mji hadi kufikia tarehe 5/2/2021 kuwa 4516 sawa na asilimia 78.62%.
Shule mpya za Sekondari zinazojengwa ni pamoja na Bombambili yenye madarasa kumi, Kisesa yenye madarasa matano na Mkangara madarasa matano. Baada ya kukamilika kwa ujenzi huo Halmashauri itaifanya Halmashauri ya Mji kuwa na shule za Sekondari 19 kutoka 16 zilizokuwepo awali, Pia ujenzi wa shule mpya ya Nyakato katika Kata ya Nyanguku utaanza mapema mwaka 2021.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa