Halmashauri ya Mji Geita, imefunga rasmi mafunzo ya Usimamizi wa maswala ya fedha, Miradi na Utawala Bora kwa Watendaji na Wenyeviti wa Mitaa na Vijiji, yaliyofanyika kwa siku mbili kuanzia jana tarehe 01.02.2022 hadi leo tarehe o2.02.2020 katika ukumbi wa mikutano wa Gedeco.
Mafunzo hayo yameshirikisha Wenyeviti wa Mitaa na Vijiji 149 kutoka katika Mitaa na Vijiji ndani ya Halmashauri ya mji Geita ambao ndio Watendaji Wakuu ngazi ya Mtaa na Kijiji
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo leo mgeni Rasmi Bi. Zahara Michuzi ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Geita, amewataka Watendaji wote kuyatumia mafunzo hayo vizuri katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ya utoaji wa huduma kwa Wananchi.
Aidha Bi. Zahara amesisitiza na kuagiza uchapakazi, uwajibikaji na uwazi, kusimamia ulinzi na usalama, suala la maadili kwa watumishi wote, kusimamia usafi wa mazingira, kuzuia mifugo inaranda randa hovyo, kusoma mapato na matumizi ya Mitaa na Vijiji.
Bi. Zahara ameendelea kusisitiza na kuagiza upandaji wa miti kwa wananchi na Taasisi zilizopo ndani ya Vijiji na Mitaa husika, kuhakiki vibali vya ujenzi, kuanza michakato ya sensa ukusanyaji wa mapato na uibuaji wa vyanzo vipya vya mapato
Naye Afisa Utumishi wa Halmsahauri ya Mji Geita Bi. Thecla Gasembe, amesema mafunzo yaliyotolewa kwa Watendaji na Wenyeviti wa Mitaa ni kuwasaidia watendaji hao katika utekelezaji wa utoaji wa huduma bora kwa Wananchi
Pia Bi. Thecla amesema kuwa maelekezo na maagizo yote yaliyotolewa na Mkurugenzi wa Mji yanasisitizwa pamoja na mkataba waliopewa leo, lakini pia mafunzo haya kimsingi yana tija kubwa sana katika Halmashauri yetu.
Naye Katibu wa Watendaji katika mafunzo hayo Bw. Billian Sabato, akisoma ufupisho wa mafunzo hayo kwa mgeni rasmi amesema kuwa mafunzo yamekamilika na kuahidi kuyatumia vyema katika kazi zao za utoaji wa huduma kwa jamii.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Watendaji katika mafunzo hayo Bw. Dua Issa Kaburi, amepongeza mafunzo hayo kutolewa kwa watendaji hao kwani yatasaidia kwa kiasi kikubwa kubadili mfumo wa utendaji wao katika utoaji wa huduma bora kwa Wananchi.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa