Maafisa Watendaji Kata na Watumishi wametakiwa kuzingatia haki za raia wakati wa utoaji huduma kwa Jamii kwani imeonekana kuna baadhi ya maeneo haki hizo zinaminywa.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Geita Yefred Myenzi ametoa kauli hiyo wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa Watendaji na Wakuu wa Idara na kusisitiza viongozi hao wanatakiwa kuwa mfano wa kuigwa katika utoaji wa Haki.
Migogoro mbalimbali imeonekana kuwa changamoto katika maeneo tofauti tofauti Mkoani Geita, huku kwa upande wa Manispaa ya Geita Veronica, Hamadi Hussen Afisa Mtendaji Kata ya Kalangalala Chasama Afisa Mtendaji kata ya Buhalahala na Cathbeth Byabato Afisa Ustawi halmashauri ya Manispaa wa Geita wakigusia changamoto ya ukatili wa kijinsia na watoto wanaoishi katika mazingira magumu huku wakiona namna bora ya kuitatua baada ya mafunzo hayo.
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Hamisi Mjanja, amesisitiza suala la ushirikishaji katika uongozi ili kudumisha Demokrasia.
Manispaa ya Geita ni halmashauri ya 6 katika utoaji wa elimu hiyo, ikianza Geita DC, Bukombe, Chato, Mbogwe, Nyang’hwale na kukamilisha Geita Manispaa.
MATUKIO KATIKA PICHA
TD
CF
GH
GJHH
GJHB
GH
JHK
HH
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa